• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 9:50 AM
MAWAIDHA YA KIISLAMU: Umuhimu wa kutoa zakah katika jamii ya Kiislamu

MAWAIDHA YA KIISLAMU: Umuhimu wa kutoa zakah katika jamii ya Kiislamu

Na HAWA ALI

MOJA katika mipangilio ni kwamba kila kitu kilichopo ni Chake Allaah (Subhaanahu Wata’ala) na kumilikiwa na binadamu kama ni amana tu.

Amana hii hukabidhiwa kwa muda tu na kwa masharti na jinsi Allaah (Subhaanahu Wata’ala) Anavyotaka. Na katika moja ya mipangilio yake (Subhaanahu Wata’ala) ni Zakaah.

Neno Zakaah katika lugha ya kiarabu lina maana ya tohara, baraka, kutakasa na pia kuongeza.

Kisheria ni kile kiwango cha mali ambacho Waislamu wanapaswa kukitoa ikiwa kama ni haki yake Allaah (Subhaanahu Wata’ala) na kuwapa wanaostahiki.

Ni nguzo ya tatu katika nguzo tano za Kiislamu na amri Yake Allaah (Subhaanahu Wata’ala) ambayo ni wajibu kutekelezwa na kila Muislamu mwenye uwezo.

Zakaah si malipo, kodi, ada au takrima bali ni moja katika taasisi iliyoasisiwa na Allaah (Subhaanahu Wata’ala) ili kuleta uwiano katika neema Alizowajaalia waja wake.

Umuhimu wa Zakah

Inawakumbusha Waislamu kwamba kila walichojaaliwa ni neema kutoka kwake (Subhaanahu Wata’ala) na Allaah Hupenda neema zake kutumika jinsi alivyoagiza.

Mwenye kutoa Zakaah hutekeleza ibadah na mojawapo katika nguzo kuu za Kiislamu. Ibada ambayo kila Muislamu mwenye uwezo huwajibika nayo kuitekeleza. Mwenye kupewa Zakaah hupewa ikiwa ni kama moja ya shukrani Zake Allaah (Subhaanahu Wata’ala) na miongoni mwa haki zake.

Wenye kutoa Zakaah ndio waliojaaliwa sifa ya waumini wa kweli kwa mujibu wa Qur’ an.

Radhi za Allaah

Zakaah humsaidia muislamu katika maisha ya kidunia. Kwa kupata radhi Zake Allaah (Subhaanahu Wata’ala. Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda. Na chochote mtakachokitoa basi hakika Allaah anakijua. [Imraan: 92], kuzidisha baraka na kuongezeka kwa mali.

Mshikamano

Zakah inawashikamanisha watu pamoja kwa kuwa ni aina ya mshikamano wa kijamii.

Matajiri wataendeleza hisia za upendo, na huruma kwa masikini. Masikini wataendeleza hisia za utii, heshima, kufanya kazi kwa umakini kwa matajiri.

Hisia za choyo, chuki na kijicho zitatulizwa na hata kutokomezwa.

Matajiri hawatowadhulumu masikini na kuwaweka chini ya masharti; masikini hawaendeleza hisia za udhalilishaji, utumwa, kinyongo na husuda kwa matajiri.

Yafuatayo yanaelezwa katika hadith: “Moyo humfanya mtu ampende anayemtendea ihsani na kumfanya mtu amchukie anayemtendea uovu.”

You can share this post!

TAHARIRI: Serikali itoe ARVs bora kwa watoto ili kuzuia vifo

EACC yaahidi kuchuja vikali wawaniaji 2022

T L