• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 6:50 AM
USHAURI NASAHA: Katika elimu na maisha mtu hutiwa makali na wanaotangamana naye

USHAURI NASAHA: Katika elimu na maisha mtu hutiwa makali na wanaotangamana naye

Hali hii inawiana fika na maisha ya binadamu. Mshikadau yeyote katika sekta ya elimu anapojitenga na wengine huona kama mambo yanaenda vizuri asione haja ya kujikaza.

Ni kwa msingi huu inakuwa muhimu mno kutangamana na wengine mlio katika harakati moja nao ili kujifunza kila mmoja kutoka kwa mwenziwe.

Ewe mwanafunzi unahitaji kutangamana na wanafunzi wengine na kuona ni yepi unayoweza kujifunza kutoka kwao. Yamkini mbinu zao za kujifunza ni bora kuliko zako. Labda namna wanavyoupangia muda wao ni vyema zaidi kuliko unavyofanya.

Kukosa kuangazia namna wenzako wanavyopanga mambo yao ni namna ya kujipunguzia mfichuo (exposure) na ukweli ni kwamba utasalia nyuma. Si mwanafunzi tu anayepaswa kujifunza kwa mwanafunzi mwenziwe.

Mwalimu unalo jukumu pia kuhakikisha unawazuru walimu wenzako na kushauriana nao kuhusu mbinu mpya za kufundisha na kutahini, mitindo ya kuwahamasisha wanafuzi wa ngazi mbalimbali na mengineyo.

Ukiuchukua mkondo huu utatokea kujifunza mengi yatakayokufanya uwe mwalimu bora zaidi.Nawe mzazi hujasazwa katika harakati hii.

Jitahidi kadri ya uwezo wako kujua mbinu wanazozitumia kulipa karo za wanao kwa wakati.

Je, wanawashawishi vipi wanao na kushiriki nao mazungumzo na mashauriano ya kuyaboresha mahusiano yao? Hatua hii itakuwezesha kuwa mzazi bora.

  • Tags

You can share this post!

Walioteuliwa na Ruto wapata idhini bungeni

GWIJI WA WIKI: Ali Attas

T L