• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
USHAURI NASAHA: Zipo taaluma tele za Kiswahili katika soko la ajira nchini

USHAURI NASAHA: Zipo taaluma tele za Kiswahili katika soko la ajira nchini

NA HENRY MOKUA

TUNAPOFIKIA kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani leo Alhamisi, kuna haja ya kutambua kwamba hii ni mojawapo ya lugha zinazokua kwa kasi zaidi ulimwenguni.

Ilivyo ada, kila kitu chema kinapokua, matarajio nayo hukua kwa kiasi sawa na kufikia ngazi mpya. Je, ewe mwanafunzi wa Kiswahili unapaswa kuwa na matarajio yap?

Kwa mujibu wa hadhi mpya kilichopewa Kiswahili katika taasisi za masomo nchini, kinaibua matumaini mengi mapya tena makubwa. Nimekuwa nikiwahimiza wanafunzi kukithamini Kiswahili tangu nijiunge na taaluma yangu hii ya ualimu. Nimezidisha juhudi zenyewe katika miaka ya hivi karibuni. Kwa nini lakini?

Ikiwa lugha rasmi sawa na Kiingereza, Kiswahili kimekuwa mbadala muhimu katika kujiunga na taaluma mbalimbali. Kwa mujibu wa Bodi ya Kuwasajili wanafunzi kujiunga na Vyuo Vikuu na vya Kadri, Kiswahili ni mojawapo ya masomo yaliyojumuishwa katika matakwa ya msingi (minimum requirements).

Mtahiniwa akifuzu vyema katika Kiswahili anajipa nafasi nzuri ya kujiunga na mojawapo katika kozi kadha wa kadha; nyingine zisizohusiana na Kiswahili moja kwa moja kama vile uhandisi.

Miongoni mwa taaluma za msingi unazoweza kujiunga nazo na kutumia Kiswahili kujikuza na kujiendeleza ni uanahabari. Uanahabari unahusisha kuandaa taarifa na kuzipererusha kupitia vifaa vya kielektroniki kama redio na runinga. Aidha, hujumuisha kuzipitisha taarifa na makala kwa njia ya magazeti kama ninavyofanya sasa hivi.

Taaluma nyingine zinazotokana na lugha ya Kiswahili ni pamoja na uandishi wa vitabu, ukalimani, kuwa mtafsiri, ualimu, sanaa ya filamu na uigizaji na uimbaji .

  • Tags

You can share this post!

Magavana wafagia akaunti za kaunti

SIKU YA KISWAHILI DUNIANI: Tutambue mchango wa watangulizi...

T L