• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 1:14 PM
Vidokezo muhimu kupunguza uharibifu wa chakula

Vidokezo muhimu kupunguza uharibifu wa chakula

NA NARGARET MAINA

[email protected]

UHARIBIFU wa chakula ni suala kuu katika jamii ya kisasa.

Uharibifu huu unaharibu au unaathiri vibaya bajeti zetu, lakini pia kutoa taswira mbaya ikizingatiwa kwamba wako baadhi ya watu ambao lau wangekipata, wangefurahia sana badala ya kuendelea kusumbuliwa na makali ya njaa.

Je, ni vipi tunavyoweza kukabili suala hili la uharibifu wa chakula?

Zingatia mambo haya muhimu ukiwa kwa nyumba yako mwenyewe:

Kuwa na vifaa sahihi

Cha kwanza kuzuia upotevu wa chakula ni kuhakikisha jikoni mwako kuna vifaa bora. Chakula mara nyingi hutupwa kwa sababu chakula kina ladha mbaya.

Angalia tarehe ya matumizi

Hii ni njia nzuri ya kupunguza upotevu, lakini inaweza kumaanisha kuwa vitu unavyoleta nyumbani kutoka kwa maduka vinaweza visidumu kwa muda mrefu kama unavyotarajia.Ikiwa kitu kitahifadhiwa kwa muda mrefu, angalia kila wakati ili kuhakikisha kuwa kitatumika kabla ya kuharibika.

Tumia orodha ya ununuzi kila wakati

Maduka makubwa yameundwa ili kutuhimiza kununua vitu tusivyohitaji, kwa hivyo kuwa na orodha kwani ndio ulinzi wako bora linapokuja suala la kukomesha upotevu wa chakula nyumbani. Ukifanya hivyo, chakula hakiwezi kuharibika kwenye jokofu au kuishia kwenye jaa kwa sababu hukununua chakula kiasi na aina usiohitaji. Ulifuata orodha ya bidhaa muhimu ulizotaka kununua.

Maandalizi ya chakula

Njia nyingine nzuri ya kupunguza upotezaji wa chakula ni kuandaa chakula. Kwa kupika kwa wingi na kula vyakula unavyovihitaji, utapata wazo bora la kile kilicho kwenye jokofu yako, hii pia ni bora ya kuokoa muda.

Kugandisha mabaki

Ikiwa unafikiri hutamaliza milo uliyotayarisha kabla haijaharibika, au una masalio kwa usiku mmoja, jokofu lako ni rafiki yako mkubwa. Ingawa kwa hakika kuna baadhi ya vyakula ambavyo haviwezi kugandishwa, idadi kubwa zaidi inaweza kuwa katika hali hiyo.

  • Tags

You can share this post!

Naibu Rais akutana na Raila

AFYA YA AKILI: Jinsi ya kuepuka msongo wa mawazo na...

T L