• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:07 PM
JUMA NAMLOLA: Naibu Rais anafahamu vyema kwamba siasa si za mashekhe na walokole

JUMA NAMLOLA: Naibu Rais anafahamu vyema kwamba siasa si za mashekhe na walokole

NA JUMA NAMLOLA

KWA yeyote aliyemsikiliza Naibu Rais William Ruto katika kaunti ya Kiambu Jumatatu, si vigumu kuona mtu anayejaribu kushika matawi ya mfa maji.

Waswahili husema mfa maji haachi kutapatapa.

Uchaguzi Mkuu utafanywa Agosti 9, zaidi ya miezi minne na nusu ijayo.

Katika siasa, siku moja ni kama mwaka na mambo yanaweza kubadilika.

Hata hivyo, hali ilivyo kwa sasa, ni dhahiri kuwa Dkt Ruto alikuwa akitarajia kupata baraka za Rais Uhuru Kenyatta.

Baraka hizo ni muhimu mno, ingawa Rais Kenyatta alitangaza wazi hadharani kuwa kura yake ni moja.

Unapoungwa mkono na rais aliye mamlakani, ujumbe unaotumwa kwa umma ni kuwa wewe unatosha.

Wapigakura wana usemi wao katika uchaguzi, lakini kauli ya kiongozi kuwa unafaa huongeza uzito katika nafasi ya mtu kuchaguliwa na wananchi.

Malalamishi ya Dkt Ruto kwamba Rais Kenyatta si mtu wa kutimiza ahadi huenda yakawa kweli kwa raia, lakini si kwa mwananchi.

Ni yeye Dkt Ruto ambaye mnamo Machi 9, 2013 katika uwanja wa michezo ya Kasarani alitoa ahadi chungu nzima.

Kwanza aliahidi kuwa utawala wa Muungano wa Jubilee wakati huo, ungetumia rasilmali vyema kujenga uchumi wa nchi. Punde alipoingia afisini, kukazuka madai ya utumizi mbaya wa ndege.

Akaahidi uwanja mmoja wa michezo katika kila kaunti. Akaahidi unga ungekuwa bei ya hasla. Unga uliuzwa kwa Sh90 kwa miezi michache tu.

Katika siasa, wanasiasa hutenda au kusema mambo ili kufurahisha. Siasa na uwakili ni kati ya taaluma ambazo kusema uongo ni sifa ya ushujaa. Kwa hivyo kama Dkt Ruto alimsaidia Rais Kenyatta kuingia uongozini na kutawala kwa miaka kumi, alionyesha wazi kuanzia 2018 kuwa uongozi mtu hujitafutia.

Siasa si za mashekhe, mapadri na walokole wengine. Unapokubaliana jambo na mwanasiasa, tambua kuwa makubaliano hayo ni kulingana na maslahi ya mmoja wenu wakati huo.

  • Tags

You can share this post!

Serikali yaondolea wadhimini wa michezo ushuru

680 kushiriki Riadha za Dunia za Ukumbini, Omanyala...

T L