• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Serikali yaondolea wadhimini wa michezo ushuru

Serikali yaondolea wadhimini wa michezo ushuru

Na GEOFFREY ANENE

WATU binafsi na kampuni zinazodhamini michezo zina sababu ya kutabasamu baada ya serikali kuamua kuwaondolea ushuru kwa fedha watakazotumia kukuza michezo nchini Kenya.

Katika taarifa kwa marais wote wa mashirikisho ya michezo, Waziri wa Michezo Amina Mohamed ameomba watu binafsi na kampuni zinazolenga kudhamini michezo na wachezaji kuhakiksha kuwa wachezaji ndio wanaonufaika katika migao hiyo.

Ili kunufaika na mpango huo, wadhamini lazima wapate kibali kutoka kwa Wizara ya Michezo na pia kufichua kiasi cha fedha wanazopanga kuwekeza katika michezo hiyo.

Waziri wa Michezo kisha atapeana ruhusa na kuwasiliana na Kamishina Mkuu wa Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru, Kenya (KRA) kupitia kwa barua.

Kwa miaka nyingi, wadhamini wamekuwa wakijiuliza kwanini michango yao ya kusaidia klabu ama mashindano haitambuliwi na KRA kuwa ni gharama.

Hatua hii inatarajiwa kuwapa wadhamini motisha ya kusaidia timu na michezo mbalimbali nchini.

Timu ya taifa ya Olimpiki 2020 ilidhaminiwa na kampuni ya bia ya East Africa Breweries inayodhamini pia Tusker FC inayoshiriki Ligi Kuu ya soka nchini.

Kampuni ya sukari ya West Kenya inadhamini Kabras Sugar RFC inayoshiriki Ligi Kuu ya raga nchini.

Klabu nyingine za soka zinazopata ufadhili kutoka kwa kampuni mbalimbali ni KCB na Posta Rangers. Kampuni ya Safaricom inadhamini gofu. Hayo ni baadhi tu ya mashirika yanayodhamini michezo nchini.

  • Tags

You can share this post!

Real wakomoa Mallorca na kufungua mwanya wa alama 10...

JUMA NAMLOLA: Naibu Rais anafahamu vyema kwamba siasa si za...

T L