• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
MOHAMED OSMAN: Mapendekezo ya Glagsow kuhusu mabadiliko ya hali ya anga yatekelezwe

MOHAMED OSMAN: Mapendekezo ya Glagsow kuhusu mabadiliko ya hali ya anga yatekelezwe

Na MOHAMED OSMAN

ILIKUWA fahari kubwa kuwaona magavana na washikadau kutoka kaunti mbalimbali wakijadili kuhusu mabadiliko ya tabianchi kwenye kongamano la ugatuzi lililokamilika wiki jana katika Kaunti ya Kitui.

Vinara hao wa kaunti walijadili kuhusu majukumu ya serikali za kaunti na ile ya kitaifa katika kukabiliana na masuala yanayochangia mabadiliko ya hali ya anga kisha kuwa na athari ya moja kwa moja katika maisha ya binadamu na viumbe wengine hai ulimwenguni.

Ukweli ni kwamba, athari ya mabadiliko ya tabianchi imechangia umaskini katika nchi mbalimbali, mafuriko, ukame na uchafuzi wa mazingira.

Kwa hivyo, ni vyema iwapo raia watapata mafunzo au hamasisho mara kwa mara kuhusu sera ambazo zinatumiwa kuhakikisha mabadiliko ya hali ya hewa hayaathiri maisha yao na jinsi wanaweza kuzuia uchafuzi wa hali ya hewa na mazingira.

Kwanza, Afisi ya kisheria ya Ombudsman ina wajibu wa kutunga sera ambazo zinafaa ziangazie njia ya kupambana na uchafuzi wa mazingira na kupendekeza adhabu kali kwa wanaohusika.

Hata hivyo, inasikitisha kuwa katika baadhi ya kaunti, utunzaji wa mazingira hauzingatiwi na uchafuzi wa mazingira ni jambo la kawaida raia wakijali tu mapato yao.

Hii ni kwa sababu wenye kampuni mbalimbali za kutengeneza bidhaa wamekuwa wakitoa hongo kwa baadhi ya wakuu wa kaunti ili kuruhusu shughuli za kuchafua mazingira.

Kati ya mapendekezo yaliyoibuka katika kongamano hilo ni nchi mbalimbali kudhibiti kiwango cha kaboni inayoishia hewani na kuhatarisha maisha ya viumbe ulimwenguni.

Hili suala la uchafuzi wa hali ya hewa na mazingira si la hapa nchini bali la ulimwengu mzima kwa jumla.

You can share this post!

Koo 7 zasaka maafikiano kabla uchaguzi

BALLON D’OR: Messi tena? Lewandowski kachezwa!

T L