• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 6:50 AM
Matumizi mbalimbali ya mtama

Matumizi mbalimbali ya mtama

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MTAMA ni miongoni mwa mazao ya chakula.

Ubora wa mtama hutokana na mtama kutunzwa vizuri shambani, kuvunwa kwa wakati, kukaushwa, kusafishwa vizuri na kuhifadhiwa vema.

Maandalizi yanayotakiwa kufanywa kabla ya kupika ni: kupepeta na kupembua, kuosha, kusaga kama unataka kupata bidhaa ya unga.

Mtama una matumizi mbalimbali:

  • Chakula cha binadamu kama vile ugali, uji, mikate na vyakula vya nyongeza vya watoto.
  • Chakula cha mifugo kama kuku, ngombe, au nguruwe.
  • Majani ya mtama hutumika kutengeneza saileji.
  • Mtama hutumika kutengeneza vinywaji kama pombe.
  • Unga wa mtama hutumika kuboresha vyakula vyenye upungufu wa protini kama muhogo.
  • Pia mmea wa mtama kinatumika kulainisha uji mzito wa mahindi, muhogo n.k., unaotumika kuwalishia watoto wadogo.

Mtama una virutubisho muhimu vinavyotakiwa katika mwili wa binadamu. Una kiasi cha wanga, nishati, nyuzi nyuzi, na mafuta karibu au sawa na mahindi au nafaka nyingine.

Mtama una madini aina ya chuma, protini kwa wingi, vitamin B complex, vitamin C na vitamin E kwa wingi. Mtama una madini ya zinki, potassium, na manganisi kwa wingi kuliko nafaka nyingine.

Sukari iliyoko kwenye mtama huyeyuka taratibu sana mwilini hivyo mtama ni chakula kinachofaa kuliwa na watu wenye magonjwa kama kisukari.

Mtama huimarisha afya ya mifupa.Magnesiamu ipo katika viwango vya juu sana kwenye mtama, ina maanisha kiwango chako cha kalsiamu kitakuwa kimedhibitiwa, kwani magnesiumu huongeza uingizwaji wa kalsiumu kwenye mwili.

Madini haya mawili pia ni muhimu kwenye maendeleo ya tishu za mifupa na kuharakisha kupona kwa mfupa ulioharibika au mifupa iliyozeeka. Hii huweza kuzuia hali kama osteoporosis na shida ya uti wa mgongo, kukufanya kuwa imara na mwenye afya kwenye umri wa uzee.

  • Tags

You can share this post!

NCIC yapiga marufuku baadhi ya maneno na msamiati katika...

Wakazi wa Murang’a wapata afueni mafuta yakijazwa...

T L