• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 12:09 PM
NCIC yapiga marufuku baadhi ya maneno na msamiati katika muktadha wa siasa

NCIC yapiga marufuku baadhi ya maneno na msamiati katika muktadha wa siasa

NA WINNIE ONYANDO

TUME ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa (NCIC) Ijumaa ilitoa orodha ya maneo 23 ambayo yamepigwa marufuku katika hafla zote za kisiasa.

Akizungumza jana Ijumaa jijini Nairobi, Mwenyekiti wa NCIC, Dkt Samuel Kobia alisema maneno hayo 23 yanafaa kuepukika kwa kuwa yanaaminika kuchochea chuki katika kampeni za kisiasa.

“Maneno hayo tuliyoyaorodhesha yatatumika kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Hii itasaidia kupambana na matamshi ya chuki nchini,” akasema Dkt Kobia.

Maneno ya Kiingereza yaliyopigwa marufuku na tume hiyo ni Fumigation ambayo inalenga wanajamii ambao si wakazi rasmi wa eneo fulani, Uncircumcised, Eliminate na Kill.

Kwa upande mwingine, maneno ya Kiswahili kama vile Kaffir, Madoadoa, Chunga Kura, Mende, Watu wa kurusha mawe, Watajua hawajui, Wabara waende kwao, Wakuja, Chinja Kaffir na Kwekwe yamepigwa marufuku katika hafla zote za kisiasa.

Maneno ya Kikuyu kama vile Kihii, Uthamaki ni witu hayafai kutamkwa, maneno ya Kimeru kama vile Mwiji na ya Kikalenjin yanayojumuisha Kimurkeldet, Otutu labotonik na Ngetiik yote yamepigwa marufuku.

Maneno Hatupangwingwi, Operashion Linda Kura na Kama noma, noma yote hayafai kutumika.

Kadhalika, tume hiyo pia inamulika vikundi 14 vya mirengo ya kisiasa ya Azimio la Umoja na Kenya Kwanza ambavyo vinaaminiwa kuendeleza matamshi ya chuki uchaguzi wa Agosti 9 ukikaribia.

Vikundi hivyo vinajumuisha Lamu County politics, Migori Revolutionalist Council, The Kalenjin Forum, The New Mamaans Borana, Voices of Change, The Marsabit County We All Want members, The Marsabit County we want, Raila Odinga for President, Group Kericho County, Baba the 5th! Inawezekana. Azimio la Umoja, UasinGishu County Forum, BUNGOMA COUNTY FORUM, Azimio la Umoja na Group Kenya.

  • Tags

You can share this post!

TUSIJE TUKASAHAU: Tungali tuna kibarua kutokomeza ukeketaji

Matumizi mbalimbali ya mtama

T L