• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Masaibu ya Baraza la Kitaifa la Mashujaa

TUSIJE TUKASAHAU: Masaibu ya Baraza la Kitaifa la Mashujaa

JUZI serikali ililipa Sh1.3 milioni, bili ya hospitali iliyochangia mkewe shujaa wa uhuru Dedan Kimathi, Mukami Kimathi, kuzuiliwa katika Nairobi Hospital.

Bi Kimathi alilazwa katika hospitali hiyo mnamo Januari 5, 2023 akiugua ugonjwa wa nimonia na matatizo mengine yanayohusiana na uzee.

Naibu Rais Rigathi Gachagua alimtembelea shujaa huyo ambapo alisema ni aibu na mateso kwa nyanya kama huyo kuzuiliwa hospitalini “ilhali ni miongoni mwa waliochangia kupatikana kwa uhuru wa taifa hili.”

“Tumelipa bili hiyo na tunamtakia afueni kamili. Hatukuwa na habari kuhusu madhila yake kwa sababu mimi na rais tumekuwa katika ziara ya eneo la Nyanza,” akasema.

Lakini Naibu Rais asije akasahau kuna Sheria kuhusu Mashujaa wa Kenya iliyotiwa saini ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta mnamo 2016, bosi wake, Dkt Ruto kama Naibu Rais.

Kutokana na sheria hiyo, kulibuniwa Baraza la Kitaifa la Mashujaa linaloongozwa na Katibu Mkuu wa zamani wa Baraza la Waislamu Nchini (SUPKEM) Adan Wachu. Mojawapo ya majukumu ya baraza hilo la mashujaa ni kushughulikia masilahi ya mashujaa lakini limekosa ufadhili wa kutosha kutoka Serikali Kuu.

  • Tags

You can share this post!

Serikali yapanga kupunguza ada ya NHIF

Raha ya wadau meli ya watalii 620 ikitia nanga

T L