• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Ujenzi wa daraja katika Mto Enziu unafanywa kwa mwendo wa kujikokota

TUSIJE TUKASAHAU: Ujenzi wa daraja katika Mto Enziu unafanywa kwa mwendo wa kujikokota

MNAMO Desemba 2021, serikali ilitenga Sh600 milioni kufadhili ujenzi wa daraja katika Mto Enziu, Mwingi ya Kati, Kaunti ya Kitui ambako watu 31 walikufa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutumbukia katika mtu huo.

Ujenzi wa daraja hilo ulianza Januari 2022 na ulitarajiwa kukamilika baada ya miezi sita.

Lakini miezi 11 baadaye, mradi huo haujakamilika na sasa wakazi wameingiwa na hofu kwamba huenda maafa mengine yakatokea msimu huu wa mvua.

Wakazi wa eneo hilo, wakiongozwa na Mbunge wa Mwingi ya Kati Gideon Mulyungi sasa wanamtaka Waziri mpya wa Uchukuzi na Miundomsingi Onemus Kipchumba Murkomen asisahau kumsukuma mwanakandarasi aliyepewa kazi hiyo alikamilishe haraka.

Aidha, wanaitaka kampuni ya Kiu Construction iliyopewa kandarasi ya ujenzi wa daraja hilo kukumbuka kwamba kazi hiyo ilinuiwa kuokoa maisha ya wakazi wanaotumia daraja hilo kuvuka kutoka eneo la Nguni hadi Nuu.

  • Tags

You can share this post!

UN, Amerika zasifu Ethiopia kwa kusitisha vita na Tigray

Mkataba wa Kenya Kwanza waumiza ANC na Ford Kenya

T L