• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
WANTO WARUI: Serikali itumie kawi ya jua kufanikisha elimu dijitali katika maeneo kame

WANTO WARUI: Serikali itumie kawi ya jua kufanikisha elimu dijitali katika maeneo kame

Licha ya juhudi za serikali kusambaza umeme nchini, bado kuna maeneo mengi ambayo hayajafikiwa na hakuna matumaini ya kupata umeme hivi karibuni.

Wanafunzi wanaosomea maeneo hayo bila shaka wako nyuma kimasomo kutokana na ukosefu wa umeme.

Hivyo basi, hata vifaa vya kidijitali ni vigumu kutumika huko.Katika mtaala mpya wa elimu CBC, masomo takriban yote yanatumia video zinazopatikana katika vifaa vya kidigitali. Baada ya kusoma darasani pamoja na walimu, wanafunzi wanaelekezwa kwa kazi za ziada kupitia vifaa vya kidijitali.

Katika sehemu za mijini ambapo kuna umeme, wanafunzi wanafanya kazi hizo vizuri sana na kuelewa masomo kwa undani. Wanafunzi walio vijijini na sehemu kame zisizo na umeme wanamalizia masomo yao pale pale kwa vitabu tu wasiwe na fursa ya kuelewa wanachosoma vyema zaidi kupitia vifaa vya kidijitali.

Tatizo hili si la kufumbiwa macho kwani linaweza kuathiri elimu pakubwa. Hii ndiyo sababu serikali inafaa kuchukua hatua za dharura ili kurekebisha jambo hili kwa manufaa ya wanafunzi wengi wanaoteseka.

Bila shaka matokeo ya mitihani inayoendelea kufanywa na wanafunzi wanaosoma mtaala wa CBC yanaonyesha wazi tofauti zilizopo kati ya wanafunzi wanaotumia vifaa vya kidijitali na wale wanaosoma wakitumia vitabu tu.Kwa kuwezesha vifaa hivi vitumike kote, serikali haina budi kufanikisha matumizi ya nguvu za jua katika shule ambazo ziko maeneo kama hayo ambako stima haipo.

  • Tags

You can share this post!

Okutoyi azamia mazoezi kupunguza makosa kabla ya W15 Nairobi

PAUKWA: Ajabu ya Tundu ‘mfu’ kuwatokea wanakijiji

T L