• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
WANTO WARUI: Wanafunzi wa Gredi 6 waandaliwe kikamilifu kwa mitihani yao

WANTO WARUI: Wanafunzi wa Gredi 6 waandaliwe kikamilifu kwa mitihani yao

NA WANTO WARUI

HATIMAYE msimu wa mitihani ya kitaifa umewadia huku maelfu ya wanafunzi wakiitayarisha kwa sababu hiyo.

Wale wa Kidato cha Nne wanajitayarisha kwa mtihani wa KCSE, Darasa la Nane kwa mtihani wa KCPE nao wale wa Gredi ya 6 ambao ndio kwanza wanafanya mtihani wao wa KPSEA wakijinoa makali.

Kati ya makundi haya matatu, walimu wanaofunza watahiniwa wa Gredi ya 6 wangali wageni katika kukabiliana na mitihani ya kitaifa hasa wakati huu ambapo mtaala wa elimu ni mpya.

Kuna uwezakano mkubwa kuwa, walimu hawajawatayarisha wanafunzi hao wa Gredi ya 6 vya kutosha.

Walimu kutoka shule nyingi wanaegemea sana kuwatayarisha wanafunzi wa Darasa la Nane huku wakisahau umuhimu wa kuwatayarisha wale wa Gredi ya 6.

Mashindano ambayo yamekuwapo kwa miaka mingi katika matokeo ya KCPE ndiyo yanayochangia katika matayarisho ya kina ya wanafunzi hao.

Hata hivyo, huenda walimu wengi wakapigwa na mshangao mkubwa kwa sababu ya matokeo ya mtihani wa KPSEA wa Gredi ya 6.

Baraza la Kitaifa la Mitihani nchini (KNEC) halina budi kuandaa mtihani wa Gredi ya 6 ambao umeafiki viwango na unaotahini kama wanafunzi wamefundishwa silabasi ipasavyo.

Hivi ni kusema kuwa, matokeo ya Gredi ya 6 yatakuwa na umuhimu mkubwa kama yale ya Darasa la Nane na yale ya Kidato cha Nne.

Walimu ambao wamepewa jukumu la kutayarisha wanafunzi wa Gredi ya 6 hawana budi kuweka mikakati mizuri kwa sababu kuna hatari ya wanafunzi hao kufeli wasipotayarishwa vyema.

Kwanza, wanafunzi hao wanafanya mtihani wa masomo 11 ambayo yameunganishwa pamoja katika karatasi nne.

Hata hivyo, masomo haya ni mengi na yanahusisha walimu wengi katika kuyafunza huku mengine yakiwa na vipindi vichache mno kwa juma.

  • Tags

You can share this post!

Unapopika, wape watoto fursa ya kujifunza kutoka kwako

9 kutoa ushahidi wa madai ya wizi wa kura Kwale

T L