• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 5:50 AM
Agala na Makokha wamaliza voliboli ya ufukweni Olimpiki bila ushindi

Agala na Makokha wamaliza voliboli ya ufukweni Olimpiki bila ushindi

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya Kenya ya voliboli ya ufukweni imekamilisha kampeni yake ya Olimpiki 2020 bila ushindi baada ya kupoteza dhidi ya Latvia kwa seti 2-0 katika mechi yake mwisho ya Kundi D jijini Tokyo, Japan, Jumamosi.

Brackcides Agala Khadambi na Gaudencia Makokha walipoteza seti ya kwanza dhidi ya Tina Graudina na Anastasija Kravcenoka kwa alama 21-6 katika dakika 13 kabla ya kujikakamua na kufikisha alama 14 katika seti ya pili iliyodumu dakika 14 ufuoni Shiokaze Park.

Wakenya hao walianza kampeni yao kwa kulimwa 2-0 (21-15, 21-9) na raia wa Brazil Ana Patricia/Rebecca mnamo Julai 26 na pia kupokea dozi sawa na hiyo mikononi mwa Waamerika Kelly Claes/Sarah Sponcil mnamo Julai 29.

Ni mara ya kwanza Kenya ilishiriki voliboli ya ufukweni kwenye Olimpiki.

Ilipata tiketi baada ya kunyamazisha Nigeria katika fainali ya Afrika mnamo Juni 27 mjini Agadir, Morocco.

Mbali na voliboli ya ufukweni, Kenya pia ilikuwa na wawakilishi katika fainali ya uogeleaji, taekwondo, ndondi, voliboli, riadha na raga ya wachezaji saba kila upande.

You can share this post!

Corona: Kagwe atoa afueni kwa kaunti 13 za magharibi mwa...

Klabu za Barcelona, Juventus na Real Madrid zaendelea...