• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Aliyekuwa mpuliza kipenga wa EPL, Mark Clattenburg, ajiuzulu kuwa Rais wa Kamati ya Marefa nchini Misri

Aliyekuwa mpuliza kipenga wa EPL, Mark Clattenburg, ajiuzulu kuwa Rais wa Kamati ya Marefa nchini Misri

Na MASHIRIKA

REFA wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Mark Clattenburg, amejiuzulu kutoka kwenye wadhifa wa kuwa Rais wa Kamati ya Marefa nchini Misri baada ya miezi mitano pekee.

Shirikisho la Soka la Misri (EFA) limethibitisha kwamba Clattenburg, 47, amejiondoa kwenye wadhifa huo na wamekubaliana na uamuzi wake wa kujiuzulu.

Clattenburg alikashifiwa na kukosolewa pakubwa wiki hii na rais wa klabu ya Zamalek club, Mortada Mansour, kupitia runinga ya Zamalek TV inayomilikiwa na kikosi hicho kilichozamishwa na Al-Ahly katika Ligi Kuu ya Misri.

Clattenburg alikwezwa ngazi kuwa mwamuzi wa mechi za EPL mnamo 2004 baada ya kupuliza kipenga katika ligi za chini kwa kipindi cha miaka mitatu. Mechi yake ya mwisho katika EPL ilikuwa kati ya Leicester City waliokomoa West Bromwich Albion 1-0 mnamo Aprili 2017.

Alikuwa pia mwamuzi wa fainali ya Euro 2016 iliyoshuhudia wenyeji Ureno wakikomoa Ufaransa 1-0. Ndiye aliyeaminiwa pia fursa ya kupuliza kipenga wakati wa fainali ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) iliyoshuhudia Real Madrid wakifunga Atletico Madrid penalti 5-3 baada ya sare ya 1-1 mwishoni mwa muda wa ziada.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Dhana ya Utamaushi inavyokuzwa katika ‘Chozi la Heri’

NGUVU ZA HOJA: Walimu wa lugha ya Kiswahili waandaliwe...

T L