• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 6:50 AM
Arsenal watoshana nguvu na Brentford kwa sare ya 1-1 katika EPL

Arsenal watoshana nguvu na Brentford kwa sare ya 1-1 katika EPL

Na MASHIRIKA

ARSENAL walipoteza fursa ya kufungua mwanya wa alama nane kati yao na nambari mbili Manchester City kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya Brentford kuwalazimishia sare ya 1-1 mnamo Jumamosi ugani Emirates.

Baada ya kutoshana nguvu kwa sare tasa katika kipindi cha pili kilichoshuhudia kombora la Ivan Toney wa Brentford likigonga mwamba wa goli la kipa Aaron Ramsdale, Arsenal walirejea ugani kwa matao ya juu katika kipindi cha pili.

Sajili mpya Leandro Trossard alifunga bao lake la kwanza kambini mwa Arsenal na kuwaweka viongozi hao wa jedwali kifua mbele kunako dakika ya 66. Hata hivyo, juhudi zake zilifutwa na Toney dakika nane baadaye kupitia krosi ya Christian Norgaard.

Hata hivyo, ilichukua muda wa takriban dakika tatu kwa bao hilo la Brentford kuthibitishwa na teknolojia ya VAR. Toney sasa amepachika wavuni mabao 15 katika EPL msimu huu na anasoma migongo ya Erling Haaland na Harry Kane.

Sare dhidi ya Brentford ni pigo kubwa kwa Arsenal ambao sasa wanajiandaa kuvaana na mabingwa watetezi Man-City mnamo Februari 15, 2023 ugani Emirates.

Huku Brentford wakishikilia sasa nafasi ya nane kwa alama 34, Arsenal walisalia kileleni mwa jedwali kwa alama 51, sita zaidi kuliko Man-City watakaokuwa wenyeji wa Aston Villa uwanjani Etihad mnamo Februari 12, 2022.

Arsenal walisajili sare dhidi ya Everton baada ya kupigwa na Man-City kwenye Kombe la FA na kukung’utwa na Everton katika pambano la EPL lililoyumbisha matumaini yao ya kujizolea taji la EPL kwa mara ya kwanza tangu 2003-04.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

TUSIJE TUKASAHAU: Sharti Ruto apate idhini ya Bunge kabla...

Shirika laangazia jinsi vijana wanavyodhulumiwa kingono na...

T L