• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 8:55 AM
Arsenal watumia Sh22.8 bilioni kujisuka upya msimu huu

Arsenal watumia Sh22.8 bilioni kujisuka upya msimu huu

Na MASHIRIKA

MATUMIZI ya Arsenal katika soko la uhamisho wa wachezaji muhula huu yamefikia Sh22.8 bilioni baada ya kikosi hicho kumsajili beki raia wa Japan, Talehiro Tomiyasu kutoka Bologna kwa mkataba wa miaka minne.

Kusajiliwa kwa Tomiyasu, 22, kuliwapa Arsenal fursa ya kumtuma Mhispania Hector Bellerin kambini mwa Real Betis kwa mkopo. Kikosi hicho cha kocha Mikel Arteta kimemkubalia pia fowadi chipukizi Reiss Nelson kujiunga na Feyenoord ya Uholanzi kwa mkopo wa msimu mmoja.

Tomiyasu aliwajibikia Bologna mara 31 katika Ligi Kuu ya Italia (Serie A) mnamo 2020-21. Kuja kwake kunatarajiwa kupiga jeki safu ya ulinzi ya Arsenal ambayo sasa iko chini ya Calum Chambers, Rob Holding, Sead Kolasinac na Cedric Soares.

Arsenal wamejishughulisha vilivyo katika soko la uhamisho muhula huu huku wakijinasia huduma za beki Ben White (Sh7.8 bilioni), kiungo Martin Odegaard (4.7 bilioni) na kipa Aaron Ramsdale (3.7 bilioni).

Bellerin, 26, alikosa kupata uhakika wa kuunga kikosi cha kwanza cha Arsenal tangu apate jeraha baya la goti mnamo 2019. Hata hivyo, alichezeshwa mara 25 katika kampeni za msimu wa 2020-21.

Nyota huyo alisajiliwa na Arsenal kutoka akademia ya Barcelona mnamo 2011 na kufikia sasa, angali na mkataba wa miaka miwili kati yake na Arsenal.

Nelson, 21, alichezea Hoffenheim ya Ujerumani kwa mkopo mnamo 2018-19 kabla ya kurejea Arsenal ambao amewawajibikia mara 48 na kufungia mabao manne.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Real Madrid wamng’oa tineja Camavinga kutoka Rennes...

CHARLES WASONGA: Si wakati mwafaka wa kuadhimisha ya Siku...