• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Real Madrid wamng’oa tineja Camavinga kutoka Rennes ya Ufaransa

Real Madrid wamng’oa tineja Camavinga kutoka Rennes ya Ufaransa

Na MASHIRIKA

REAL Madrid wamejinasia maarifa ya kiungo matata raia wa Ufaransa, Eduardo Camavinga kutoka Rennes kwa mkataba wa miaka sita.

Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 18 alikuwa katika miezi 12 ya mwisho wa mkataba wake na Rennes ya Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) iliyokuwa haitaki kumwachilia aondoke bila ada yoyote msimu ujao.

Mnamo Aprili 2019, Camavinga aliweka historia ya kuwa mwanasoka mchanga zaidi kuwahi kuwajibishwa na Rennes akiwa na umri wa miaka 16 na miezi minne pekee.

Alipata uhakika wa kuunga kikosi cha kwanza na akawajibishwa mara 60 ligini chini ya kipindi cha misimu miwili iliyopita.

Tineja huyo aliweka historia ya kuwa mchezaji mchanga zaidi kuwahi kuchezea timu ya taifa ya watu wazima ya Ufaransa tangu 1914 baada ya kuwajibishwa dhidi ya Croatia katika Uefa Nations League mnamo Septemba 2020. Alifunga bao lake la kwanza ndani ya jezi za timu ya taifa mwezi mmoja baadaye katika ushindi wa 7-1 dhidi ya Ukraine kirafiki.

Camavinga anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na Real muhula huu baada ya beki raia wa Austria, David Alaba aliyetokea Bayern Munich ya Ujerumani.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Barcelona wamsajili De Jong, Griezmann arejea Atletico

Arsenal watumia Sh22.8 bilioni kujisuka upya msimu huu