• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
BACK TO BASIC FC yajivunia vipaji tegemeo

BACK TO BASIC FC yajivunia vipaji tegemeo

NA ABDULRAHMAN SHERIFF

KUMEKUWA na malamiko mengi kuhusu kutojaribiwa kwa baadhi ya makocha wa jimbo la Pwani kupewa fursa ya kuifunza timu ya Harambee Stars lakini vilio vya baadhi ya washika dau wa sehemu hiyo, kamwe havijatiliwa maanani.

Mmoja wa makocha ambao amekuwa akitajika mno sio kuliliwa kuifunza Harambee Stars pekee bali pia timu ya Pwani iliyoko Ligi Kuu ya Kenya ya Bandari FC ni Rajab Babu ambaye amewahi kuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya soka la ufukweni ya Harambee Sand Stars na Stars U-17 na U-20.

Lakini kukosa kupata fursa hiyzo hakukumvunja moyo mkufunzi huyo kwani hamu yake kubwa ni kuhakikisha chipukizi wanainua vipaji vyao na hivyo aliunda klabu ya Back To Basic (B2B) ambayo anaendelea kukuza vijana ambao wengineo wameanza kutambulika.

Akizungumza uwanja wao wa mazoezi wa Mombasa Sports Club (MSC), Babu alisema anashukuru sana kuwa juhudi anazozifanya kwa klabu hiyo kwani zimeanza kutambulika na chipukizi wake watatu wamepata udhamini wa masomo shule ya upili ya Serani.

“Nina furaha kubwa kuona vijana wameanza kuvutia shule za upili na nina matumaini kila mwaka, watatokea wengine ambao nao watahitajika kujiunga na shule hiyo ama nyenginezo ambazo zitavutiwa na mchezo wao,” akasema mkufunzi huyo.

Wanasoka hao waliopata udhamini wa masomo katika shule ya Serani ni Nixon Charo na Hamisi Omar wanaosoma kidato cha kwanza na Don Otieno aliyeko kidato cha pili.

Babu ambaye aliwahi kusafiri na klabu ya Mombasa FC ya vijana wa umri chini ya miaka 12 hadi Lyon nchini Ufaransa kushiriki mashindano ya Danone Nations Cup yaliyohusisha timu kutoka mataifa 45 duniani mwaka 2007 anaamini vijana wake hao watafanikiwa kufikia malengo yao.

“Kwa hawa vijana, siwashirikishi kwenye mashindano ama ligi yoyote kwa sababu nataka wapate mafunzo wakiondoka wawe ni wenye kuhitajika kujiunga na klabu kubwa pamoja na shule za upili,” akasema Babu huku akisema anawaangazia wachezaji wenye umri kati ya miaka mitano hadi 16.

Anawashukuru wakuu wa MSC pamoja na wanachama kwa kuwaruhusu kukitumia mkiwanja chao kwa ajili ya mazoezi kila Jumapili na akasema klabu hiyo imekubali kwa sababu ya nia ya kuwapa watoto kutoka familia za kimasikini fursa ya kucheza kwenye viwanja vya kisasa.

“Bila ya msaada ninaopewa na MSC, nisingeweza kuwasaidia vijana hawa ambao hawana uwezo wa kulipia gharama za vifaa na kuchezea kwenye viwanja vizuri lakini hapa wanapata mahitaji yao na mafunzo yasiyokuwa na malipo yoyote,” akasema Babu.

Amewashukuru pia makocha wenzake watano ambao nao wamejitolea kusaidia kuwapa mafunzo vijana hao ambao ana uhakika baada ya miaka michache ijayo, watakuwa wakitajika na kucheza soka la hali ya juu.

Wakufunzi hao watano wanaosaidiana na Babu kuwajenga watoto hao ni Mohamed Hussein Osman, Gladys Mutisya, Kimkon Obondo, Kidzao Nyanje na Seif Rashid.

Babu alisema kuwa wachezaji walioko katika B2B wanatoka kaunti ndogo zote sita za Kaunti ya Mombasa ambazo ni Jomvu, Kisauni, Mvita, Nyali, Likoni na Changamwe.

Kocha Babu ana imani kubwa kuwa wakati utafika kwa chipukizi wake hao kuhitajika na klabu kubwa kwani amewaona wengi wao kuwa wenye vipaji vya hali ya juu ya kuwa wachezaji wenye majina makubwa.

Mwanzilishi huyo wa Back To Basic FC (B2B) ni kusaidia vijana wanainukia kupata fursa ya kuinua vipaji vyao hadi kufikia kucheza soka la kulipwa hapa nchini ama huko Ulaya.

Wanasoka hao wanaotoka sehemu mbalimbali za Mombasa na ambao wanapata mafunzo kutoka kwa Rajab Babu ambaye ni mkufunzi aliyefuzu kufunza soka akiwa na hati za mataifa mbalimbali yakiwemo yale ya Uholanzi na Brazil.

Huu ni wakati mzuri kwa chipukizi wa B2B kuchukua fursa ya mafunzo wanayopata kwa uzito ili waweze kufikia malengo yapo pamoja na yale ya wazazi wao ya kupata fursa ya kwenda ng’ambo kuchezea klabu za huko.

“Ni jambo la kutufurahisha sisi wazazi kwa Babu kuwafunza watoto wetu wa kuanzia umri wa miaka mitano hadi 16 na tumeanza kuvutiwa na jinsi Watoto wetu hawa wanavyoinuka na kuwa na vipaji vitakavyowasaidia kupata fursa ya kuchukuliwa na klabu za nje,” alisema mzazi wa mtoto wa umri wa miaka minane ambaye hakupenda kutaja jina.

Chipukizi wa Back to Basic FC (B2B) wanatarajia kunufaika pakubwa kwa ushirikiano ambao ulianza kujitokeza kati yao na FC St Pauli ya Ligi 2 Bundesliga ya nchini Ujerumani.

Back to Basic FC inayofunzwa na kusimamiwa na Rajab Babu inatarajia kunufaika pakubwa hasa kwa wanasoka wake watakaofikia umri unaohitajika na kuwa na vipaji vya uchezaji wa hali ya juu, kufikiriwa kusajiliwa na klabu hiyo ya Ujerumani.

“Nina hamu kubwa mwanangu afuatilize mafunzo anayopewa na Babu nikitarajia iko siku itafika atavutia klabu kubwa na kusajiliwa kucheza soka la kulipwa huko ng’ambo na hasa nchini Uingereza,” alisema mzazi wa mwanasoka wa timu hiyo ya B2B ya umri chini ya miaka 13.

Uhusiano baina ya klabu hizo mbili umetokana na St Pauli kuwaletea zawadi ya vifaa B2B zikiwemo mipira 102 kati ya hayo 86 ni mipya, flana 77, bukta 52, soksi 125 na bips za rangi mbalimbali 321

  • Tags

You can share this post!

Re Union yapiga moyo konde kujikaza kupanda ngazi

Madaktari 24 wafuzu MKU