• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 3:16 PM
Barcelona wajitwalia huduma za beki raia wa Brazil, Emerson

Barcelona wajitwalia huduma za beki raia wa Brazil, Emerson

Na MASHIRIKA

BARCELONA wamesajili mchezaji wa tatu muhula huu baada ya kumtwaa beki raia wa Brazil, Emerson Royal mwenye umri wa miaka 22 kutoka Real Betis ya Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga).

Emerson aliwahi kuwa kuchezea Barcelona alipoagana na kikosi cha Atletico Mineiro cha Brazil mnamo Januari 2019. Hata hivyo, alitumwa kwa mkopo hadi kambini mwa Betis kwa mkopo kabla ya klabu hiyo kumpokeza mkataba wa kudumu mwishowe.

Chini ya kocha Ronald Koeman, Barcelona walikuwa tayari wamejinasia maarifa ya wanasoka Sergio Aguero na Eric Garcia kabla ya Emerson kutua ugani Camp Nou. Aguero na Garcia waliingia katika sajili rasmi ya Barcelona bila ada yoyote baada ya mikataba yao na Manchester City ya Uingereza kutamatika.

Kiungo matata wa Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi, Georginio Wijnaldum, anatarajiwa pia kujiunga na Barcelona bila ada yoyote kufikia mwisho wa mwezi Juni 2021.

Emerson amewajibikia Betis katika jumla ya mapambano yote na kufungia kikosi hicho jumla ya mabao matano na kuchangia mengine 10. Ndiye mwanasoka aliyesakata idadi kubwa zaidi ya michuano katika msimu wa 2020-21 chini ya kocha Manuel Pellegrini aliyewaongoza Betis kuambulia nafasi ya sita kwenye La Liga na hivyo kufuzu kwa soka ya Europa League.

Emerson amewakilisha Brazil katika mapambano kadhaa ya chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 na miaka 23 kabla ya kuwajibishwa kwa mara ya kwanza katika timu ya watu wazima mnamo Novemba 2019.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Muller na Hummels wachezea Ujerumani kwa mara ya kwanza...

Beatrice Chebet anyakua taji la Montreuil nchini Ufaransa