• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:07 PM
Bayern na Lewandowski waweka rekodi mpya za ufungaji wa mabao katika Bundesliga

Bayern na Lewandowski waweka rekodi mpya za ufungaji wa mabao katika Bundesliga

Na MASHIRIKA

ROBERT Lewandowski alifunga bao lake la 300 katika Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) mnamo Jumamosi.

Nyota huyo raia wa Poland alisaidia waajiri wake Bayern Munich kutikisa nyavu za wapinzani kwa mara ya 66 mfululizo ligini na hivyo kukomoa Cologne 4-0.

Lewandowski aliyecheka na nyavu za wenyeji wao mara tatu, alifungulia Bayern ukurasa wa mabao katika dakika ya tisa huku jingine likifumwa wavuni na Corentin Tolisso.

Ushindi huo wa Bayern uliwawezesha kufungua mwanya wa alama sita kati yao na nambari mbili Borussia Dortmund kileleni mwa jedwali la Bundesliga. Dortmund waliocharaza Freiburg 5-1 mnamo Jumamosi, sasa wana pointi 40, tisa zaidi kuliko Hoffenheim wanaofunga orodha ya nne-bora. Bayer Leverkusen wanashikilia nafasi ya tatu kwa alama 32.

Baada ya kufunga bao katika mechi 66 mfululizo ligini, Bayern kwa sasa wanashikilia rekodi ya kutikisa nyavu za wapinzani katika idadi kubwa zaidi ya michuano kwa mfululizo kwenye Bundesliga. Walivunja rekodi yao ya zamani ya kushinda mechi 65 mfululizo kati ya Februari 2018 na Februari 2020.

Kwa kufikisha mabao 300 kwenye Bundesliga, Lewandowski ndiye mchezaji wa kwanza kufikisha rekodi hiyo tangu nguli Gerd Muller ambaye sasa ni marehemu afanye hivyo mnamo 1976.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Raila adai Ruto alichangia kufeli kwa Jubilee

Mitaa mitatu Mukuru yakosa maji kwa kipindi cha wiki nzima

T L