• Nairobi
  • Last Updated May 14th, 2024 10:01 PM
Benzema aongoza Real Madrid kuzamisha chombo cha Alaves kwenye La Liga

Benzema aongoza Real Madrid kuzamisha chombo cha Alaves kwenye La Liga

Na MASHIRIKA

KARIM Benzema alifunga mabao mawili na kuongoza Real Madrid kuchabanga Alaves 4-1 katika mchuano wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) msimu huu chini ya kocha Carlo Ancelotti.

Mechi hiyo ilinogeshwa pia na fowadi Gareth Bale aliyerejea Real muhula huu baada ya kuhudumu kambini mwa Tottenham Hotspur kwa mkopo mnamo 2020-21.

Eden Hazard alichangia bao la kwanza ambalo Real walifungiwa na Benzema katika dakika ya 48 kabla ya Nacho Fernandez kufunga goli la pili dakika nane baadaye.

Benzema alifunga bao jingine katika dakika ya 62 kabla ya Jose Luis Mato kurejesha Alaves mchezoni kupitia mkwaju wa penalti. Vinicius Jr alifungia Real bao la nne mwishoni mwa kipindi cha pili.

Mechi hiyo iliwapa Real jukwaa la kumwajibisha beki David Alaba kwa mara ya kwanza tangu ajiunge nao kutoka Bayern Munich. Difenda huyo raia wa Austria ndiye alichangia goli lililofumwa wavuni na Vinicius.

Kurejea kwa kocha Ancelotti kambini mwa Real kunatarajiwa kufufua makali ya Bale aliyejipata akisugua benchi chini ya Zinedine Zidane kiasi cha kurejea Spurs kwa mkopo kwa mwaka mmoja. Hadi alipochezeshwa dhidi ya Alaves, mechi ya mwisho kwa Bale kusakatia Real ilikuwa dhidi ya Mallorca mnamo Juni 2020.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Tammy Abraham atua Italia kukamilisha uhamisho wake hadi AS...

Wanasiasa watoroka mazishi ya Chidzuga kwa kuzuiwa kupiga...