• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Canada waingia fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1986

Canada waingia fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1986

Na MASHIRIKA

CANADA walitinga fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1986 baada ya kuponda Jamaica 4-0 mnamo Jumapili usiku.

Ushindi huo jijini Toronto unawapa Canada uhakika wa kukamilisha kampeni za kufuzu ndani ya nafasi ya tatu miongoni mwa mataifa ya Shirikisho la Amerika Kaskazini, Kati na Caribbbean (Concacaf). Canada walinogesha fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya mwisho miaka 36 iliyopita nchini Mexico. Walidenguliwa mapema kwenye fainali hizo baada ya kuvuta mkia bila kufunga bao lolote kundini.

Wakicheza dhidi ya Jamaica ugani BMO Field mnamo Jumampili, Canada walipata mabao kupitia kwa Cyle Larin, Tajon Buchanan, Junior Hoilett na Adrian Mariappa aliyejifunga. Amerika, Mexico, Costa Rica na Panama ni miongoni mwa mataifa yanayopigania nafasi mbili nyinginezo kutoka shirikisho la Concacaf za kufuzu kwa Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar.

Kikosi kitakachoambulia nafasi ya nne katika orodha ya mataifa manane ya Concacaf kitalazimika kushiriki mchujo dhidi ya mshindi wa mechi itakayokutanisha Solomon Islands na New Zealand za Shirikisho la Soka la Oceania.

You can share this post!

Fainali ya mpira wa vikapu ya wanaume kati ya Ulinzi na KPA...

Vipusa wa Chelsea waponda Leicester na kutua kileleni mwa...

T L