• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Cherotich na Kipng’etich watifulia wenzao kivumbi mbio za makinda za South Rift

Cherotich na Kipng’etich watifulia wenzao kivumbi mbio za makinda za South Rift

Na AYUMBA AYODI

FAITH Cherotich na Ronald Kipng’etich kutoka eneo la Kipkelion waliachia vumbi wapinzani wao kwenye mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji wakati wa mashindano ya eneo la South Rift ugani Kericho Green mnamo Jumamosi.

Mashindano hayo ni ya mchujo wa kuingia timu ya Kenya ya Riadha za Dunia za Under-20 zitakazofanyika jijini Nairobi mwezi Julai.

Benson Kiplang’at kutoka Nakuru na Ezra Kiplang’at (Bomet) walitawala mbio za mita 5,000 za makundi mawili ya kwanza, mtawalia.

Mercy Chepkemoi kutoka Nakuru aliacha hoi wapinzani wake katika mbio za mita 5,000 za kinadada.

Bernard Yegon (Nakuru) na Isca Chelangat (Kipkelion) waling’ara katika mbio za mita 3,000 za wanaume na wanawake, mtawalia.

Kipng’etich, ambaye alinyakua nishani ya shaba kwenye Riadha za Afrika 2018 katika mbio za mita 2,000 kuruka viunzi na maji, alitumia dakika 8:50.57 kubeba taji la mbio za kuruka viunzi na maji. Aliwabwaga wapinzani kutoka Bomet, Kibet Chepkwony (8:53.90) na Simon Kiprop (8:59.24).

“Nalenga kushinda mchujo wa kitaifa ili nipate kuwakilisha Kenya katika mashindano ya chipukizi kabla ya kupanda ngazi ya mashindano ya watu wazima mwaka ujao,” alisema Kipng’etich.

Cherotich, ambaye yuko katika kidato cha kwanza katika Shule ya Upili ya Sugutek katika kaunti ya Kericho, alikamilisha kitengo chake kwa dakika 11: 09.22. Alifuatwa na wenzake kutoka Kipkelion, Diana Chepkemoi (11:57.69), Triza Cherotich (12:12.98) na Sharon Chepkemoi (12:20.35).

Everline Chepkoech na Daniel Kiplagat waliandikisha kasi ya juu katika vitengo vyao vya mbio za mita 800 baada ya kukamilisha mizunguko hiyo miwili kwa dakika 2:08.19 na 1:51.34, mtawalia.

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

You can share this post!

JAMVI: Wazee wa Pwani wanakosa sauti ya kunguruma kisiasa

Watu wa Ruto waona moto