• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:07 PM
Chris Oguso Cup yaleta burudani Vihiga

Chris Oguso Cup yaleta burudani Vihiga

NA RUTH AREGE

KWA miaka 11 sasa, michuano ya Chris Oguso imekuwa ikinogesha sherehe za krismasi na mwaka mpya kupitia soka katika kaunti ya Vihiga.

Ongusu ni mchezaji wa zamani wa Kenya ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa timu ya Police Fc ya Ligi Kuu ya Wanaume Nchini (FKF-PL), anatumia mashindano haya kuwapa vijana nafasi kujitangaza katika soka.

Michuano hiyo hufanyika katika Kijiji cha Mahanga, Eneo la Mungoma katika Kaunti ya Vihiga. Ni sehemu inayopokea takriban watu 3,000, wengi wao wakiwa ni vijana wa kiume na wa kike ambao wamemaliza elimu yao ya sekondari.

Mashindano hayo yalianza tarehe 10 mwezi huu yakiwa na timu 32. Timu ya Kidundu United ilitwaa ubingwa wa Mwaka huu baada ya kuwapiga Lakers Fc 3-0 kwenye fainali siku ya Alhamisi.

Kiungo Vincent Ogopa alifunga mabao mawili naye Michael Ake akafunga bao la tatu.

Nao Sportive FC kupitia Eugene Esilaba wakamaliza nafasi ya tatu baada ya ushindi 1-0 dhidi ya Silver Strikers.

Kidundu walienda nyumbani na Sh300,000 na kikombe cha kibinafasi. Nafasi ya pili na tatu walituzwa Sh200,000 na Sh100,000 mtawalia. Washindi hao pia walituzwa jezi, medali na mipira.

“Hii ni motisha kwetu, timu yetu ina vijana wadogo na wachanga sana. Kupitia nafasi hizi wanatumia kuonyesha talanta zao wakiwa na imani kuwa siku moja jua litawaangazia,” alisema nahodha wa Kidundu Mohammed Said.

Mikel Ake alituzwa mwanasoka bora wamashindano hayo, Ian Dancan wa Kidundu aliibuka mlinda lango bora nae Benson Kamalic wa Sportive akashinda kiatu cha dhahabu na mabao 12.

Oguso  amevutia ufadhili kutoka kwa kampuni ya kamari ya Betika. Michuano hiyo imevutia timu kutoka maeneo bunge ya Vihiga, Hamisi, Sabatia, Luanda na Emuhaya.

Kando na ratiba, Oguso kwa miaka mingi amewaalika wachezaji bora, waliopo na waliostaafu, ili kuzitia moyo timu za wenyeji, zikiongozwa na gwiji wa zamani Joe Kadenge.

Mwaka huu, wachezaji wa zamani wa Harambee Stars wakiwemo viungo Joshphat Murila na George Sunguti pamoja na mwenyekiti wa timu ya Sukari ya Nzoia Evas Kadenge pia walihudhuria shindano hilo.

“Mashindano kama haya yanawapa wachezaji wa mashinani nafasi ya kuonyesha talanta zao. Kuna baadhi ya wachezaji wa Ligi Kuu ambao wametoka kwenye shindano hili. Kuna wengine pia tutawasajili kwenye ligi ikiwa watakubali,” alisema Kadenge.

  • Tags

You can share this post!

Faida na manufaa ya tunda la tini (fig)

Mtoto mvulana aliyeng’olewa macho analindwa na serikali,...

T L