• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Faida na manufaa ya tunda la tini (fig)

Faida na manufaa ya tunda la tini (fig)

NA MARGARET MAINA

[email protected]

TINI mbichi kwa kawaida huwa laini kutoka katikati ikiambatana na mbegu.

Umbile hili la kipekee huifanya kuwa tunda kubwa kufurahia jinsi lilivyo. Tini ni sehemu ya lishe yenye afya kama mbadala wa sukari ya mezani.

Tini ni chanzo kizuri cha kalsiamu na potasiamu. Madini haya yanaweza kufanya kazi pamoja ili kuboresha msongamano wa mifupa, ambayo inaweza, kwa upande wake, kuzuia hali kama vile osteoporosis. Uchunguzi unaonyesha kuwa lishe yenye potasiamu, haswa, inaweza kuboresha afya ya mfupa na kupunguza shida ya mifupa.

Tini ni chanzo asili cha sukari, nyuzi mumunyifu, na madini mengi. Madini moja ambayo ni muhimu sana kwetu sote ni chuma. Tini safi na kavu ni chanzo bora cha chuma. Tini ni ghala la virutubisho kama potasiamu, kalsiamu, magnesiamu, shaba, vioksidishaji kama vitamini A na Vitamin L ambayo inaweza kuchangia afya kwa ujumla na siha.

Faida za kiafya za tini:

1: Husaidia kuondoa kuvimbiwa

Tini zilitumiwa tangu azali kama dawa ya kizamani ya kutibu kuvimbiwa na hivyo kusaidia kurutubisha matumbo. Tini hufanya kazi kama laxative asili kutokana na sifa yake ya kuwa na nyuzi mumunyifu. Kwa hivyo, hurahisisha mchakato wa matumbo yenye shida.

2: Inaweza kupunguza uzito

Tini yenye nyuzinyuzi nyingi inaweza kuwa kitafunio kizuri au vitafunio vya asubuhi, haswa kwa wanaotaka kupunguza uzani. Ukila tini zilizokaushwa zinaweza kukufanya ujisikie umeshiba kwa muda mrefu na hii inaweza kusaidia kuweka mapengo marefu kati ya mlo mmoja hadi mwingine.

3: Inaweza kudhibiti shinikizo la damu

Ulaji wa vyakula vya haraka umekuwa ukiongezeka siku hadi siku; mazoea yanayoweza kusababisha matatizo ya shinikizo la damu. Shinikizo la damu mara nyingi husababisha kutokuwa na usawa wa viwango vya potasiamu katika mwili wako. Tini zikiwa chanzo kizuri cha potasiamu, zinaweza kuboresha kiwango cha potasiamu na hivyo kudhibiti shinikizo la damu.

4: Inaweza kuboresha usawa wa usagaji chakula

Tini ni chanzo kikubwa cha prebiotics, kumaanisha kuwa inaweza kusaidia kuboresha mchakato wa usagaji wa chakula na afya ya jumla ya utumbo. Kuwa na nyuzinyuzi nyingi, pia huongeza wingi kwenye choo chako, hivyo kuwezesha haja kubwa kupita kawaida.

5: Inaweza kuboresha afya ya moyo

Uwepo wa nyuzinyuzi nyingi na potasiamu husaidia kuondoa mafuta ya ziada kutoka kwa mwili na shinikizo kutoka kwa moyo. Hii inaweza kusaidia sana kuboresha afya ya moyo wako. Pamoja na kazi hizi mbili, Tini pia huwa na mchango muhimu wa kusaidia kupunguza lehemu mbaya.

  • Tags

You can share this post!

Hazina ya Hasla sasa yamulikwa

Chris Oguso Cup yaleta burudani Vihiga

T L