• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 12:11 PM
Commander Okoth atinga nusu-fainali ya ndondi za Urusi

Commander Okoth atinga nusu-fainali ya ndondi za Urusi

Na AYUMBA AYODI
Mkenya Nick “Commander” Okoth ameingia nusu-fainali ya mashindano ya masumbwi ya makumbusho ya Konstantin Kototkov mjini  Khabarovsk, Urusi.
Okoth alizoa ushindi kwa wingi pointi dhidi ya Sergey Kishko kutoka Ukraine katika uzani wa unyoya mnamo Alhamisi. Majaji wote watano walimpa Okoth ushindi wa alama  29-28, 30-27, 30-27, 30-27 na 30-27.
Okoth sasa atalimana na mwenyeji Ovik Oganisyan kutafuta tiketi ya fainali hapo Ijumaa, huku Mkenya mwingine Elly Ajowi akipepetana na Mamadiyar Saydrahimov kutoka Uzbekistan katika robo-fainali ya uzani wa “Super heavy”.
Ushindi wa Okoth ulipatikana muda mchache baada ya mshindi wa nishani ya shaba ya Jumuiya ya Madola, Christine Ongare na bingwa wa taifa wa uzani wa “bantam”  Elizabeth Akinyi kubanduliwa katika raundi ya kwanza ya vitengo vyao.
Ongare alishindwa kwa wingi wa alama na Diana Garishnaya kutoka Estonia naye  Akinyi akaambulia kichapo sawa na hicho dhidi ya Maria Moronto kutoka Jamhuri ya  Dominican.
Shirikisho la Ndondi zisizo za malipo duniani  (AIBA) linatumia mashindano hayo kuandaa mabondia waliofuzu kushiriki michezo ya Olimpiki mjini Tokyo nchini Japan.
Serikali na Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki Kenya (NOC-K) wamefanikisha ziara ya kikosi cha mchezo wa ngumi cha Kenya maarufu kama Hit Squad.
  • Tags

You can share this post!

Liverpool waajiri kocha wao wa zamani, Matt Beard

Rangers yalenga rekodi ya kukamilisha msimu bila kulimwa