• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 8:50 AM
Congo yazoa pointi zote tatu kwa kuishinda Kangemi Allstars FC

Congo yazoa pointi zote tatu kwa kuishinda Kangemi Allstars FC

NA ABDULRAHMAN SHERIFF

CONGO Boys FC jana ilijihakikishia pointi zote tatu za Ligi ya Taifa Daraja la Kwanza ilipoifunga Kangemi Allstars FC kwa bao 1-0 kwenye mechi kali iliyochezwa uwanja wa Serani Sports mjini Mombasa, Jumamosi Machi 13, 2021.

Mechi hiyo iliyokuwa ya kupendeza kwa dakika zote 90 za mchezo, timu zote hizo za Congo na Kangemi zikionyeshana ubabe wa mchezo mzuri ila ilichokosa ni mashabiki ambao hawakuruhusiwa kuishuhudia kutokana na vikwazo vya janga la Covid-19.

Congo Boys ilijipatia bao la pekee la ushindi lilitingwa nyavuni na Hussein Abdulmalik kunako dakika ya 57. Bao hilo lilitokea kwenye vurumani langoni mwa Kangemi na baada ya kipa Peter Mageto kuondoa hatari ya kiki la Twalib Hassan, Abdulmalik akatinga nyavu.

Kocha wa Congo Boys, Abdul Nassir amewasifu wanasoka wake kwa kujituma na kusema kuna mwamko mpya katika kikosi chake na akawataka mashabiki wawe na subira kwani anatarajia matokeo ya mechi zijazo yatakuwa mazuri.

“Tumesajili mchezaji mmoja na tuna mpango wa kusajili wachezaj wengine wawili kuimarisha kikosi chetu ili tuweze kupanda ngazi hadi kwenye nafasi nzuri,” akasema Nassir huku akiwataka waamuzi watumie haki wanapochezesha mechi hizo.

Naye mkufunzi wa Kangemi Allstars, Dickson Amugasha amesema ni kutokana na uchofu wa safari kwani walifika saa kumi na moja siku moja kabla ya kucheza mechezo huo na hivyo uchofu ni mojawapo ya sababu wanasoka wake hawakucheza mchezo wao wa kawaida.

Naye hakusita kuwalaumu baadhi ya waamuzi ambao anadai huwa wanapendelea timu za nyumbani na kumtaka Rais wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) Nick Mwendwa kupanga marefarii wazuri wenye vipaji zaidi kushughulikia mechi za ligi hiyo.

“Ninaamini kama marefarii watakuwa wazuri na wa kutumia haki, ligi hii itakuwa ni bora zaidi kwani timu nyingi ni nzuri na zenye wachezaji wenye tajriba za kucheza soka la hali ya juu,” akasema Amugasha.

Timu ya Congo Boys inajitayarisha kukutana na Gor Mahia kwenye mechi ya Raundi ya timu 64 ya mashindano ya Betway Cup itakayopepetwa uwanja wa Mbaraki Sports Club hapo Machi 28. Lakini Congo imetaka FKF ipange mechi hiyo uwabnja wao wa Serqani Sports.

You can share this post!

WHO yapuuzilia mbali ‘madhara’ ya chanjo ya...

Ombi klabu za Pwani ya Afrika Mashariki zirudishe ushusiano...