• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 7:50 AM
WHO yapuuzilia mbali ‘madhara’ ya chanjo ya AstraZeneca

WHO yapuuzilia mbali ‘madhara’ ya chanjo ya AstraZeneca

Na AFP

GENEVA, Uswisi

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) Ijumaa lilisema hakuna haja ya kusitishwa kwa utoaji wa chanjo ya Covid-19 aina ya AstraZeneca kutokana na tashwishi kuhusu usalama wake kutoka kwa mataifa kadha ya Ulaya.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, WHO ilisema Kamati yake ya Ushauri kuhusu Chanjo, inatathmini data zinazowasilishwa kuhusu usalama wa chanjo hiyo.

Lakini likasema kuwa kufikia sasa hakuna ushahidi wa kuonyesha kuwa chanjo ya AstraZeneca inasababisha matatizo ya kuganda kwa damu.

Mnamo Jumatano, mataifa ya Denmark, Norway, Iceland, Austria, Estonia miongoni mwa mengine barani Ulaya yalisitisha, kwa muda, chanjo hiyo baada ya watu kadhaa kulalamikia kukumbwa na tatizo la damu kuganda.

Lakini Ijumaa Msemaji wa WHO Margaret Harris akasema: “Tuendelee kutumia AstraZeneca masuala kuhusu usalama wake yanapochunguzwa. Hata hivyo, kufikia sasa data ambazo tumepokea hazijapata uhusiano wowote kati ya chanjo hii na kuganda kwa damu.”

TAFSIRI: CHARLES WASONGA

You can share this post!

Man-City kumsajili Joao Felix wa Atletico ili kuziba pengo...

Congo yazoa pointi zote tatu kwa kuishinda Kangemi Allstars...