• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 6:50 AM
Esse Akida atuzwa kiatu cha dhahabu kwa kuibuka mfungaji bora nchini Uturuki

Esse Akida atuzwa kiatu cha dhahabu kwa kuibuka mfungaji bora nchini Uturuki

NA AREGE RUTH

MSHAMBULIAJI wa Harambee Starlets Esse Akida, ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Wanawake nchini Uturuki msimu wa 2021/22 akiwa na timu ya PAOK Thessaloniki.

Akida, 26, anatajwa kuwa mmoja wa washambuliaji mahiri wa Starlets na alituzwa kiatu cha dhahabu baada ya kufanikiwa kufunga mabao 17 katika mechi 18 alizocheza za ligi.

Mchezaji huyo wa zamani wa mabingwa mara tatu Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL), Thika Queens, alituzwa mnamo Jumatatu usiku katika tuzo za 41 za Chama cha Wanasoka wa Kulipwa na Wanasoka Wanawake (PSAPP) zilizoandaliwa katika Ukumbi wa Tamasha wa Athens nchini Uturuki.

“Kwanza niruhusu niwashukuru watu wa Ugiriki na PSAPP nzima waliofanikisha hili. Kutambua uchezaji mzuri kutoka kwa wanasoka wanawake si jambo ambalo kila mtu hufanya katika mchezo ambao unatawaliwa zaidi na wanaume,’ alisema Akida.

“Wachezaji wenzangu, makocha na benchi zima la ufundi na mashabiki wa PAOK asanteni sana kwa kutupa moyo. Kwa familia yangu huko Kenya, hili ni tuzo lenu ninyi, bila mchango wenu katika maisha yangu, sidhani kama ningekuwa hapa leo nikitoa hotuba hii,” aliongezea Akida.

PAOK ndio mabingwa mara 16 Ligi Kuu ya Wanawake ya Uguriki. Mwaka 2002, Akida alijiunga na Moving The Goalposts (MTG) ya Kenya. Mwaka 2016 huko Valencia, Uhispania alituzwa kuwa mfungaji bora wa Mashindano ya Soka ya Wanawake ya COTIF.

Mnamo Oktoba 2018, Akida alihamia klabu ya Ligat Nashim ya Israeli FC Ramat HaSharon. Februari 2020, alijiunga na Be?ikta? J.K. nchini Uturuki. Baada ya kuonekana katika mechi mbili za ligi mlipiko wa virusi vya homa ya Korona ulichangia dili hiyo kushindikana.

Akiwa anaipigia timu ya Ramat, Akida, alifanya vizuri zaidi katika safu ya ushambuliaji, alitumika zaidi kama beki wa pembeni kutokana na kuwa majeruhi wengi kikosini wakati huo. Lakini hata hivyo alifanikiwa kufunga mabao manne na kutoa pasi tano za mabao katika mechi 19 alizocheza.

Mwezi Februari mwaka huu, chini ya Kamati ya Mpito ya Shirikisho la Soka nchini (FKF), kocha wa Starlets Alex Alumirah, alimjumuisha kwenye timu ya taifa baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kwa kile kilichodaiwa kuwa alikuwa msaliti.

Alimirah alimjumuisha kwenye kikosi cha muda kwa ajili ya mechi ya kufuzu michunao ya Wanawake ya Mataifa Bingwa Barani (AWCON) dhidi ya Crested Cranes ya Uganda.

You can share this post!

Mabaki ya watu waliozikwa miaka 5,000 yapatikana Ziwa...

Ufugaji mbwa wa ulinzi wamlipa tangu aache kazi ya matatu

T L