• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 1:24 PM
Everton wakomoa West Ham ligini na kuweka hai matumaini ya kufuzu kwa Europa League

Everton wakomoa West Ham ligini na kuweka hai matumaini ya kufuzu kwa Europa League

Na MASHIRIKA

FOWADI Dominic Calvert-Lewin amewataka wanasoka wenzake kambini mwa Everton kujituma na kujiamini zaidi wakati ambapo kampeni za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu zinaelekea kutamatika.

Bao la Calvert-Lewin liliwavunia Everton ushindi wa 1-0 dhidi ya West Ham United mnamo Jumapili na kuweka hai matumaini yao ya kufuzu kwa soka ya bara Ulaya msimu ujao.

Baada ya kushikilia nafasi ya nne jedwalini kwa kipindi kirefu hadi mwanzoni mwa mwaka huu wa 2021, Everton waliteremka hadi nambari nane baada ya kusajili ushindi mara sita pekee kutokana na jumla ya michuano 18.

Bao la Calvert-Lewin dhidi ya West Ham lilikuwa lake la 16 kufikia sasa ligini msimu huu. Aidha, maamuzi ya kocha Carlo Ancelotti kuwajibisha mabeki watatu wa kati yalizaa matunda ikizingatiwa jinsi kikosi chake kilivyocheza kwa kubana sana hadi mwishoni mwa mchezo baada ya kupata bao katika dakika ya 24.

Ushindi huo ulikuwa wa pili mfululizo kwa Everton kusajili baada ya kuwapiga Arsenal 1-0 katika mchuano wao uliopita. Everton kwa sasa wanashikilia nafasi ya nane kwenye msimamo wa jedwali kwa alama 55, moja pekee nyuma ya Tottenham Hotspur na tatu nyuma ya West Ham ambao pia wamesakata mchuano mmoja zaidi kuliko masogora wa Ancelotti.

Kichapo kutoka kwa Everton ni pigo kubwa kwa kocha David Moyes wa West Ham ambaye amekuwa na matarajio makuu ya kuongoza waajiri wake kufuzu kwa soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu ujao sawa na alivyowahi kufanya na Everton mnamo 2005.

Baada ya Newcastle kutandika Leicester City 4-2 ligini, sasa ni pengo la alama tano pekee ndilo linalowatenganisha West Ham na Leicester wanaofunga orodha ya nne-bora kwa alama 63 huku zikisalia mechi tatu pekee kwa kampeni za msimu huu kukamilika.

Kufuzu kwa soka ya Europa League kutakuwa afueni na kitulizo kwa Moyes na kikosi chake cha West Ham ambacho kwa sasa kimeshinda mechi 11 za ugenini katika EPL msimu huu.

West Ham kwa sasa wanajiandaa kupepetana na Brighton uwanjani Amex mnamo Mei 15 huku Everton wakipangwa kuvaana na Aston Villa mnamo Mei 13 kabla ya kuwaalika Sheffield United siku tatu baadaye.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

West Brom washuka ngazi kutoka EPL baada ya kupepetwa na...

St Johnstone kuonana na Hibernian kwenye fainali ya...