• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Fernandinho atia saini mkataba mpya wa mwaka mmoja kambini mwa Manchester City

Fernandinho atia saini mkataba mpya wa mwaka mmoja kambini mwa Manchester City

Na MASHIRIKA

KIUNGO na nahodha wa Manchester City, Fernandinho Luiz Roza, 36, amerefusha muda wa kuhudumu kwake ugani Etihad baada ya kutia saini mkataba mpya wa mwaka mmoja.

Nyota huyo raia wa Brazil alijiunga na Man-City kutoka Shakhtar Donetsk mnamo 2013 na akasaidia miamba hao kushinda mataji manne ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) na sita ya League Cup.

Fernandinho alikuwa sehemu ya kikosi cha Man-City kilichozidiwa ujanja na Chelsea kwenye fainali ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo Mei 2021 jijini Porto, Ureno.

“Katika fikira zangu, nahisi kwamba kazi kubwa na muhimu zaidi kutoka kwangu nikiwa Man-City bad haijafanyika,” akasema sogora huyo ambaye mkataba wake wa awali na Man-City ulikuwa utamatike rasmi mnamo Juni 30, 2021.

“Hiyo ndiyo maana nimeamua kusalia Etihad kwa mwaka mmoja zaidi ili kusaidia klabu kufikia mengi ya malengo yake,” akaongeza sogora huyo.

Man-City walimpa Fernandinho utepe wa unahodha mnamo Septemba 2020 baada ya kupendekezwa na idadi kubwa ya wanasoka wenzake ugani Etihad kuwa mrithi wa David Silva aliyeyoyomea Real Sociedad waliomsajili kwa mkataba wa miaka miwili mwishoni mwa msimu wa 2019-20.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Dalili za upungufu wa maji katika ngozi

Uruguay kuvaana na Colombia nao Brazil kuonana na Chile...