• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 10:50 AM
Frankfurt kukutana na West Ham kwenye nusu-fainali ya Europa League baada ya kung’oa Barcelona

Frankfurt kukutana na West Ham kwenye nusu-fainali ya Europa League baada ya kung’oa Barcelona

Na MASHIRIKA

EINTRACHT Frankfurt walikomoa Barcelona 3-2 katika mchuano wa mkondo wa pili wa robo-fainali ya Europa League uliowakutanisha ugani Camp Nou mnamo Alhamisi usiku.

Ushindi huo uliwezesha kikosi hicho cha Ujerumani kubandua Barcelona ya Uhispania kwa jumla ya mabao 4-3 kwa kuwa mchuano wa mkondo wa kwanza ulikamilika kwa sare ya 1-1 ugani Deutsche Bank Park mnamo Aprili 7, 2022.

Frankfurt walianza mechi ya mkondo wa pili kwa matao ya juu huku wakijipa uongozi wa 3-0 kufikia dakika ya 67. Klabu hiyo sasa itakutana na West Ham United ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwenye nusu-fainali ya Europa League msimu huu.

Penalti ya Filip Kostic iliwaweka Frankfurt kifua mbele katika dakika ya nne kabla ya Rafael Borre kupachika wavuni bao la pili dakika 32 baadaye. Kostic alizamisha kabisa chombo cha Barcelona kunako dakika ya 67 baada ya kushirikiana vilivyo na Borre.

Sergio Busquets alipachika wavuni bao la kwanza la Barcelona katika dakika ya 90 kabla ya Memphis Depay kufunga penalti sekunde chache baadaye. Frankfurt walikamilisha mechi wakiwa na wachezaji 10 pekee baada ya Evan Ndicka kuonyeshwa kadi nyekundu mwishoni mwa kipindi cha pili.

Frankfurt walishinda taji la Europa League mara ya mwisho mnamo 1980.

You can share this post!

Burnley wamtimua kocha Sean Dyche

Ushindani mkali kushuhudiwa mechi za KWPL

T L