• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
Ghost Mulee kupigwa jeki na kuwasili kwa Olunga

Ghost Mulee kupigwa jeki na kuwasili kwa Olunga

Na GEOFFREY ANENE

MSHAMBULIAJI matata Michael ‘Engineer’ Olunga anatarajiwa kujiunga na Harambee Stars wakati wowote kwa mechi za kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Uganda na Rwanda.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF), wachezaji wote tisa kutoka ligi za kigeni waliotiwa na kocha Jacob ‘Ghost’ Mulee watarejea nyumbani Agosti 30.

Wachezaji hao ni kipa Ian Otieno (Zesco United, Zambia) na mabeki Joseph Okumu (KAA Gent, Ubelgiji), Eric Ouma (AIK, Uswidi). Pia, kuna viungo Richard Odada (Red Star Belgrade, Serbia), Duke Abuya (Nkana, Zambia), Duncan Otieno (Lusaka Warriors, Zambia), Eric Johanna (Jonkopings Sondra, Uswidi) pamoja na washambuliaji Michael Olunga (Al Duhail, Qatar) na Masud Juma (Difaa Hassani El Jadidi, Morocco).

Stars itaanza kampeni yake ya kuingia Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Uganda Cranes hapo Septemba 2 jijini Nairobi kabla ya kusafiri jijini Kigali kulimana na Amavubi mnamo Septemba 5 katika mechi hizo za Kundi E ambalo pia liko na Eagles ya Mali. Hakuna yeyote katika kundi hili amewahi kushiriki Kombe la Dunia.

Katika viwango bora vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) vya washiriki wa kundi hili, Mali inaongoza katika nafasi ya 60 ikifuatiwa na Uganda (84), Kenya (104) na Rwanda (127).

  • Tags

You can share this post!

Wazee waidhinisha Waiguru awanie ugavana tena 2022

Agizo Shirika la Huduma za Feri lifidie kampuni Sh5.2...