• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 10:50 AM
GUMZO: Auba hana raha tena Chelsea baada ya kutemwa UEFA

GUMZO: Auba hana raha tena Chelsea baada ya kutemwa UEFA

IMEKUSANYWA NA CECIL ODONGO

MSHAMBULIZI Pierre-Emerick Aubameyang anakaribia kuondoka Chelsea kuelekea Los Angeles inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani (MLS).

Raia huyo wa Gabon mwenye umri wa miaka 33 ameshindwa kung’aa kambini mwa The Blues tangu ajiunge nao kutoka Barcelona kipindi kirefu cha uhamisho Agosti iliyopita.

Baada ya kusajili kwa fujo mastaa kadha katika kipindi kidogo cha uhamisho mwezi jana, Chelsea iliondoa jina la Aubameyang katika orodha ya wachezaji watakaoisakatia Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Washambulizi waliotwaliwa na Chelsea juzi na kutiwa kwenye orodha hiyo ya wanasoka 25 kuchukua nafasi ya Auba ni Joao Felix, Mykhailo Mudryk and Enzo Fernandez.

Watatu hao wamedidimiza nafasi ya Aubameyang kikosini.

Kulingana na taarifa kwenye jarida la Le 10 Sport, Ufaransa, Chelsea wamekubali kumtoa Aubameyang kwa mkopo akasakatie Los Angeles ya Marekani, kwa muda uliosalia msimu huu ukamilike.

Ripoti hizo zinasema Auba amehiari mpango huo kwani nia yake ni kupata nafasi ya kucheza.

Aubameyang alitua Chelsea mwanzoni mwa msimu huu baada ya kununuliwa kwa amri ya Thomas Tuchel, ambaye alifutwa kazi kama mkufunzi wa timu hiyo wiki chache tu baada ya msimu kuanza.

Auba amefunga mabao matatu pekee tangu atue kutoka Barca nchini Uhispania.

Aidha, fomu yake duni imemshuhudia akichezea Chelsea mara 17 pekee.

Hakuwa kwenye kikosi cha Chelsea kilichoagana sare tasa na Fulham wiki jana katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Badala yake alionekana na nduguye jijini Milan, Italia.

Msimu mpya wa Los Angeles unaanza baadaye mwezi huu Februari huku mechi yao ya kwanza ikiwa dhidi ya LA Galaxy mnamo Februari 26.

  • Tags

You can share this post!

NYOTA WA WIKI: Brennan Johnson

Ukame kusukuma bei ya umeme juu – Waziri

T L