• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:04 PM
Izmir Racing kurejea ulingoni katika duru ya pili ya mashindano ya kitaifa ya Autocross

Izmir Racing kurejea ulingoni katika duru ya pili ya mashindano ya kitaifa ya Autocross

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya madereva ya Izmir Racing imetangaza itarejea ulingoni katika duru ya pili ya mashindano ya kitaifa ya Autocross yaliyodhaminiwa na benki ya KCB, hapo Februari 14.

Madereva hao walikosa raundi ya kwanza Januari 24 katika eneo la Karen Waterfront.

Duru ya pili itaandaliwa katika uwanja utakaotumiwa kwa Mbio za Magari Duniani za Safari Rally katika shamba la kituo cha michezo cha kimataifa cha Kasarani.

Madereva wa Izmir, ambao wamejizolea sifa kwa kupaisha magari, watalenga kurejea kwa kishindo baada ya kuwa nje muda mrefu.

Wataongozwa na Shalien Mughal atakayeshiriki kitengo cha 2WD Turbo, huku kakaye Sahir “Sarry” Mughal na binamu llyun Mughal wakiwania mataji katika vitengo vya 2WD Non-Turbo na Bambino, mtawalia.

Shalien, ambaye aliwahi kuibuka mshindi wa 2WD Turbo, amesema kuwa timu hiyo ina hamu kubwa kushiriki mashindano ya kwanza tangu janga la virusi vya corona livuruge msimu uliopita kutoka Machi 2020.

Shaz Esmail almaarufu Coach ndiye pekee kutoka timu ya Izmir aliyeshiriki raundi ya kwanza mtaani Karen.

Timu nyingine ambazo zimetangaza kushindana uwanjani Kasarani ni pamoja na Decko Racing ikiongozwa na Kirit Rajput (Subaru Impreza GC8), Kiana Rajput (Polaris 150cc), Yuvraj Rajput (Magibug 500cc) na Wayne Fernandes.

Lovejyot Singh, Eric Bengi na bingwa mtetezi wa kitengo cha 4WD Sahib Omar pia wapo.

Mashindano haya yanafuata masharti ya afya ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

  • Tags

You can share this post!

Wito mchezo wa magongo upewe nafasi sawa na kandanda,...

Omanga na wenzake wapata afueni