• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 7:50 AM
Wito mchezo wa magongo upewe nafasi sawa na kandanda, netiboli, voliboli

Wito mchezo wa magongo upewe nafasi sawa na kandanda, netiboli, voliboli

Na RICHARD MAOSI

HUENDA Wakenya wengi hawajawahi kusikia kuhusu mchezo wa magongo, ambao kwa kawaida hushirikisha timu mbili zenye wachezaji sita katika kila upande.

Kulingana na desturi zake washiriki huvalia mavazi meupe wakiwa wamezingira mpokeaji wa mipigo anayesimama katikati ya uwanja kuondosha mpira wa gongo.

Awali ulichezwa Uingereza katika mataifa ya theluji karne ya 18 kabla ya kujumuishwa katika michuano ya jumuia ya madola pamoja na olimpiki .Kenya imekuwa ikitoa wawakilishi kila mwaka kushiriki mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Hata hivyo katika eneo la Bonde la Ufa, Rift Valley Sports Club inayopatikana katika mji wa Nakuru ina historia ndefu kuhusu mchezo huu.

Aidha mchezaji anahitajika kuzingatia kiwango kikubwa cha usalama wake hasa kichwa na miguu.Lazima ajisitiri vyema ili kuepuka dhoruba kali za kipira hiki kigumu.

Kwa upande mwingine mashabiki hawafai kupita mita 20 mduara kutoka katikati ya uwanja.

Ni kwa sababu hiyo Rift Valley Sports Club walianzisha mashindano ya East African Cup, nchini ili kuwapatia motisha wachezaji kadhaa waliojitokeza kushiriki, katika juhudi zao kusaka mataji na vyeti angalau wapate kitu cha kujivunia.

Ushindani mkali kutoka kwa timu ya Nairobi Sports Club, ambayo inajivunia wachezaji wanaotamba kwa kumiliki wachezaji mahiri ndio walikuwa wakitoa ushindani kwao.

Mbali na Rift Valley Sports Club kuwasilisha taifa katika olimpiki zaidi ya mwongo mmoja uliopita,inaonekana kuwa mashabiki wameanza kuupokea mchezo huu vyema.

Mmoja wa wachezaji chipukizi ambaye alizungumza na Taifa Leo ni Asbel Tanui kutoka Chuo Kikuu Cha Egerton eneo la Njoro, Kaunti ya Nakuru.

Asbel analenga kuja kuwakilisha Kenya katika miaka ya baadaye katika mchezo huu ambao bado haujazoa mashabiki wa kutosha.

Janga la corona lilisababisha shughuli za michezo kusitishwa na hivyo hajakuwa akifanya mazoezi kwa muda mrefu.

“Naomba Wizara ya Michezo kupatia magongo nafasi sawa kama vile kandanda, voliboli au netiboli ili kukuza talanta nyingi kuanzia mashinani,”akasema.

Asbel anasema amekuwa akishiriki michuano ya nyumbani tu ,wala hajapata mialiko wa kushiriki katika ngome ya kimataifa, ambayo anaamini itamsaidia kunoa weledi wake.

Kando na kualika timu mbalimbali kujipima nguvu na hatimaye kujitambua,kila mara hasa wanaposhiriki michuano ya nyumbani na ugenini,ushindani mkali unazidi kuwapatia ubora usiokuwa na mfano.

Japo ufadhili ni kizungumkuti hadi leo kwa timu kadhaa hasa za mashinani,serikali haijajitokeza kadamnasi kuangazia hali halisi ya mambo nyanjani.Wachezaji wengi bado wanataabika wakitafuta wahisani,huku wachache wanaojitokeza wakiweka masharti magumu

Nakuru Rift Valley Sports Club ndiyo ngome ya michezo inayowakutanisha wachezaji wengi wanaoshiriki mchezo huu. Angalau mara moja kila mwezi.

Klabu zinazoshiriki huhusisha wanafunzi wa shule za msingi na za upili. Kwa mfano kuna Strathmore, Rift Valley Rhinos, Kongoni na Mombasa Coast.

Kwa sasa wanasherehekea kwa kuhitimisha zaidi ya nusu karne tangu kituo hiki maalum kiasisiwe 1967. Wachezaji wengi wamekuwa wakimiminika hapa kujinoa.

You can share this post!

Nation FC yaanza mazoezi ya Betway Cup na msimu mpya,...

Izmir Racing kurejea ulingoni katika duru ya pili ya...