• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:35 AM
Je, Ufaransa itapenya ngome ya Morocco?

Je, Ufaransa itapenya ngome ya Morocco?

NA JOHN ASHIHUNDU

MECHI ya nusu-fainali baina ya mabingwa wa Kombe la Dunia Ufaransa na Morocco inazidi kuvutia hisia kabla ya kung’oa nanga, huku timu zote zikiwa na matumaini ya kupata ushindi ugani Al Bayt leo Jumatano usiku na kufuzu kwa fainali.

Morocco ambao wameweka historia kama timu ya kwanza kutoka Afrika kutinga nusu-fainali wamefungwa mabao matatu tu tangu mashindano hayo yaanze, baada ya kuvuruga vigogo wa Croatia, Ubelgiji, Canada, Uhispania na Ureno.

Ni mechi inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali, ikikumbukwa kwamba kikosi hicho cha kocha Walid Regragui kinajivunia mastaa kadhaa wakiwemo washambuliaji matata- Kylian Mbappe na Oliver Giroud ambao kwa pamoja wamefunga mabao tisa.

Kadhalika, kuna Ousmane Dembele na Antoine Griezmann wanaotarajiwa kuvuruga ngome ya Morocco ambayo imekuwa imara daima.

Morocco kwa upande mwingine, huenda wakajibwaga uwanjani bila mabeki hodari Nayef Aguerd aliyekosa kucheza dhidi ya Ureno kutokana na jeraha la msuli. Mwenzake, Romain Saiss alitolewa wakati wa mechi hizo baada ya kutatizwa na jeraha la mguu.

Watakaopewa nafasi na kocha Walid Regragui kucheza kwenye safu ya ulinzi watakuwa na kibarua kigumu kukabiliana na washambuliaji matata wa kikosi cha Didier Deschamps.

Hakim Ziyech na Sofiane Boufal wanatarajiwa kuanza kama mawinga kwenye mechi hiyo, wakati mashambuliaji yakiongozwa na Youssef En-Nesyri.

Mastaa hao wanatarajiwa kuitatiza ngume ya Ufaransa itakayooongozwa na Jules Kounde akisaidiana na Theo Hernandez na Dayot Upamecano.

“Tayari tumewasoma na tuko tayari kabisa kuwakabili,” alisema Kounde ambaye huchezea klabu ya Barcelona nchini ya Ligi Kuu ya La Liga nchini Uhispania.

Wachezaji kadhaa wa Morocco waliumia kwenye mechi ya robo-fainali dhidi ya Ureno ambayo waliibuka na ushindi wa 1-0, lililofungwa na Youssef En-Nesyi.

Mechi yao dhidi ya Uhispania iliamua kupitia kwa mikwaju ya penalti, kabla ya baadaye kupata wakati mgumu dhidi ya Ureno hasa katika kipindi cha pili.

Ufaransa hawana matatizo ya majeraha kikosini, na huenda wakawa na kazi rahisi katika pambano la leo.

  • Tags

You can share this post!

Namwamba atangaza matumizi ya pufya kuwa tishio kwa Kenya

Atlas Lions ina nafasi kubwa ya kutinga fainali

T L