• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 3:16 PM
Atlas Lions ina nafasi kubwa ya kutinga fainali

Atlas Lions ina nafasi kubwa ya kutinga fainali

NA MASHIRIKA

DOHA, Qatar

KABLA ya fainali hizi kuanza nchini hapa, hakuna aliyeipa Atlas Lions nafasi ya kufikia umbali huu wa nusu-fainali, lakini mbali na hatua hiyo kubwa waliopiga, timu hiyo kutoka Afrika Kaskazini ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye Kundi F, mbele ya Croatia, Ubeligiji na Canada.

Lakini aliyekuwa nahodha wa Super Eagles ya Nigeria, Sunday Oliseh anasema Morocco inaweza kuichapa Ufaransa na kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia fainali itakapofanyika ugani Al Bayt mjini Al Khor, Jumapili.

“Morocco ina kikosi kinachoelewana vyema katika sehemu zote. Ombi langu ni washinde Kombe la Dunia,” alisema kiungo huyo aliyewakilisha Nigeria katika fainali mbili za Kombe la Dunia.

Kocha Alberto Zaccheroni pia alikuwa na matumaini kwamba Morocco ina uwezo mkubwa wa kuibuka mabingwa mwaka huu, hasa baada ya kuibandua Ureno kwa 1-0 na kufuzu kwa nusu-fainali.

Oliseh ambaye ndiye kocha mkuu wa SV 19 Straelen ya Ujerumani alizipongeza timu zote zilizowakilisha Afrika katika mashindano ya mwaka huu, baada ya kila timu kuandikisha ushindi.

Mwanasoka huyo mstaafu aliyechezea klabu za Juventus, Borussia Dortmund mna Ajax aliisaidia Nigera kutwaa ubingwa wa Afrika mnamo 1996 na taji la Olimpiki pia mwaka huo.

Tangu Kombe la Dunia lianze mnamo mwaka 1930, ni timu tatu tu za Afrika zilikuwa zimefika hatua ya robo-fainali na ambazo ni Cameroon mnamo 1990 nchini Italia, Senegal (2002, Japan/Korea Kusini) na Ghana (2014 nchini Brazil na 2022, Qatar), lakini Morocco imeweka rekodi ya kukumbukwa milele baada ya kuwa nchi ya kwanza ya bara Afrika kutinga nusu-fainali.

Atlas Lions walifika katika hatua hiyo baada ya kuitandika Ureno 1-0 lililofungwa na Youssef En-Nesyi, baada ya awali kuanza kwa sare ya 0-0 dhidi ya Croatia, wakaichapa Ubelgiji 2-0 na kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Canada katika hatua ya makundi.

Katika kiwango cha cha 16-Bora, Morocco waliibwaga Uhispania 3-0 kupitia kwa mikwaju ya penalti baada ya mechi hiyo kumalizika kwa sare ya 0-0 katika muda wa dakika 120.

Timu pekee nje ya bara Ulaya na Amerika Kusini kutinga hatua ya nusu-fainali ya mashindano haya ni Amerika mnamo 1930 na Korea Kusini mnamo 2002.

TAFSIRI: JOHN ASHIHUNDU

  • Tags

You can share this post!

Je, Ufaransa itapenya ngome ya Morocco?

Matumizi mbalimbali ya zaatari almaarufu Thyme

T L