• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 7:47 PM
Kenya Open ya kulenga shabaha kwa bastola yavutia nchi 10

Kenya Open ya kulenga shabaha kwa bastola yavutia nchi 10

Na AYUMBA AYODI

MATAIFA 10 yamethibitisha kushiriki mashindano ya kiwango cha tatu ya Kenya Open ya ulengaji shabaha kwa kutumia bunduki katika eneo la Losesia kaunti ya Samburu mnamo Juni 18-19, 2022.

Rais wa shirikisho la mchezo huo humu nchini (KSSF) Shoaib Vayani amefichua kuwa miamba Uingereza, Afrika Kusini na Misri wameingia mashindano hayo.

Mataifa mengine yaliyotoa ithibati kuwania ubingwa ni Ghana, Senegal, Zimbabwe na Uganda kutoka Afrika na Uhispania na Uswidi kutoka Ulaya.

Vayani alikuwa akizungumza wakati wa kuzinduliwa kwa mashindano hayo uliofanywa katika uwanja wa Shaba.

Alisema kuwa KSSF imealika mataifa 106. Uzinduzi huo ulihudhiriwa na mwenyekiti wa shirikisho la mchezo huo kimataifa (IPSC) Memba Kariuki na Meneja wa uwanja wa Shaba, Joseph Kamari. Alifichua kuwa mashindano hayo yanahitaji Sh15 milioni.

“Mafanikio ya kuandaa mashindano hayo ya Kenya Open yatatusaidia kuomba mashindano ya kiwango cha nne ama mashindano ya dunia siku za usoni,” alisema Vayani.

Kamari alisema kuwa mashindano hayo yatapiga jeki utalii.

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

  • Tags

You can share this post!

Man-City na Liverpool bado unyo kwa unyo katika EPL baada...

Jimi Wanjigi amtaka Rais Kenyatta ajitetee kuhusu...

T L