• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 12:05 PM
Barcelona wanyonga Sevilla na kutinga fainali ya Copa del Rey

Barcelona wanyonga Sevilla na kutinga fainali ya Copa del Rey

Na MASHIRIKA

BARCELONA walibatilisha kichapo cha 2-0 walichopokezwa na Sevilla katika mkondo wa kwanza wa nusu-fainali za Copa del Rey kwa kusajili ushindi wa 3-0 katika marudiano yaliyosakatiwa uwanjani Camp Nou mnamo Machi 3, 2021.

Ushindi huo ulikatia Barcelona ya kocha Ronald Koeman tiketi ya kunogesha fainali ya Copa del Rey msimu huu.

Martin Braithwaite aliwafungia Barcelona bao la tatu lililowawezesha kufuzu katika dakika ya 95 baada ya Ousmane Dembele na Gerard Pique kucheka na nyavu za Sevilla katika dakika za 12 na 90 mtawalia.

Ililazimu refa kutafuta mshindi wa mechi hiyo katika kipindi cha dakika 30 za ziada baada ya dakika 90 za kawaida kushuhudia Barcelona wakiongoza kwa 2-0, matokeo sawa yaliyovunwa na Sevilla katika mkondo wa kwanza.

Lucas Ocampos alipoteza penalti kwa upande wa Sevilla walioshuhudia kiungo wao Fernando Reges akionyeshwa kadi nyekundu mwishoni mwa kipindi cha pili, sekunde chache kabla ya Pique kufungia Barcelona goli la pili na kufanya mambo kuwa jumla ya 2-2.

Barcelona ambao kwa sasa wanalenga kutwaa taji la Copa del Rey kwa mara ya 31, watakutana sasa na mshindi wa nusu-fainali ya pili kati ya Athletic Bilbao na Levante. Wawili hao watavaana Machi 4, 2021 uwanjani Ciutat de Valencia baada ya kuambulia sare ya 1-1 katika mkondo wa kwanza uliochezewa Bilbao.

Maandalizi ya Barcelona kwa gozi lililowakutanisha na Sevilla yalivurugwa na tukio la kutiwa nguvuni kwa aliyekuwa rais wao, Josep Maria Bartomeu mnamo Machi 1 huku ofisi za maimba hao wa soka ya Uhispania zikipekuliwa na wapelelezi ugani Camp Nou.

Bartomeu aliyejiuzulu mwanzoni mwa msimu huu wa 2020-21, anatuhumiwa kutumia mamlaka yake vibaya na kushiriki ufisadi akiwa mamlakani.

Barcelona wanatarajiwa kufanya uchaguzi wa rais mpya mnamo Machi 8 ambapo watamchagua ama Joan Laporta, Victor Font au Toni Freixa. Watatu hao ndio wanaowania nafasi hiyo.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Kivumbi kuendelea miongoni mwa klabu tatu za kwanza Ligue 1

Rangers ya kocha Steven Gerrard sasa watia mkono mmoja...