• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:31 PM
Klabu 18 kukutana na waziri Namwamba

Klabu 18 kukutana na waziri Namwamba

NA JOHN ASHIHUNDU

WAZIRI wa Michezo, Ababu Namwamba kesho Alhamisi atakutana na viongozi wa klabu 18 za Ligi Kuu ya Kandanda Nchini kujadili hali ya baadaye ya mchezo huo kwa ujumla.

Shughuli za soka nchini zimevurugwa kwa kiasi kikubwa kufuatia marufuku ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) miezi tisa iliyopita, na mkutano wa kesho unatarajiwa kutoa mapendekezo kuhusu hali hiyo.

Tarehe rasmi ya kuanza kwa msimu mpya haijulikani tangu muda wa Kamati ya Mpito umalizike mwezi uliopita, lakini Afisa Mkuu wa Kenya Premier League Limited, Jack Oguda amethibitisha kwamba timu zote zimekubali kuhudhuria mkutano huo utakaofanyika katika afisi za Wizara ya Michezo, asubuhi.

“Niliagizwa na mwenyekiti wa klabu hizo, Ambrose Rachier na kufikia timu zote 18 na zote zimekubali kuhudhuria kikao cha kesho,” aliongeza Oguda.

Hata hivyo, habari zilizofikia Taifa Leo zilisema kwamba mkutano huo hautajumuisha wawakilishi wa FKF chini ya Nick Mwendwa.

Mkutano huu umekuja siku chache tu kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar, ambazo zimepangwa kufanyika kuanzia Novemba 8 hadi Disemba 20.

Baada ya kuchukuwa uadhifa wa kuongoza Wizara ya Michezo, Namwamba amekuwa akikutana na washikaji dau wa soka kutafuta njia za kushawishi Fifa irudishe Kenya katika mashindano ya kimataifa.

Kenya ilitolewa katika mashindano ya kimataifa mnamo Februari baada ya Serikali kupiga marufuku kamati ya Mwendwa Novemba mwaka uliopita.

Mwendwa ambaye aliamua kukaa kando, baada ya uchgunguzi kuhusu matumaini mabaya ya pesa za shirikisho hilo, anaendelea kujisafisha kuhusiana na madai kwamba alihusika katika ghashfa hiyo.

  • Tags

You can share this post!

Hofu ya usaliti yatishia kusambaratisha Azimio

Uvumbuzi: Trekta inayotumika kwenye mashamba madogo

T L