• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 6:21 PM
Kocha aliyetumia miereka kunoa wanasoka wa Sagan Tosu astaafu

Kocha aliyetumia miereka kunoa wanasoka wa Sagan Tosu astaafu

Na GEOFFREY ANENE

Hatimaye kocha Kim Myung-hwi ameondoka Sagan Tosu anayochezea Mkenya Ismael Dunga baada ya uchunguzi dhidi ya mbinu zake za kupiga wachezaji miereka mazoezini kukamilika.

Ripoti zilisema Agosti kuwa raia huyo wa Korea Kusini alitumia mamlaka yake vibaya dhidi ya vijana wake. Mchezaji, ambaye jina lake liliwekwa siri, alitoa dai hilo kwa Shirikisho la Soka Japan akisema kuwa Kim,40, alitumia ukatili na lugha chafu wakati wa kuwaelekeza.

Kim aliwahi kusimamishwa kazi mwezi Juni kwa mechi tatu alipopiga mwereka mchezaji mmoja wakati wa mazoezi. Sagan, ambayo iliajiri mshambuliaji Dunga mwezi Januari 2021 kwa kandarasi ya miaka miwili, ilichunguza Kim na kuona hakuna haja ya kumuadhibu zaidi na ikamkubalia kurejea kazini Agosti 14.

Hata hivyo, shirikisho lilifanya uchunguzi zaidi na kuipa Sagan fursa ya kuchukua hatua zinazofaa. Hapo Desemba 20, 2021, Sagan imetangaza katika tovuti yake kuwa Kim ameamua kustaafu. Kocha huyo amekuwa Sagan tangu 2011 alipoichezea kwa mwaka mmoja kabla ya kutwikwa majukumu ya kukuza makinda halafu kufanywa kocha mkuu mnamo Oktoba 2018.

You can share this post!

Spurs na Liverpool nguvu sawa katika EPL

Ndoto la straika huyo ni kuvalia chatu cha Messi

T L