• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Kocha Graham Potter aanza maisha Chelsea kwa sare ya 1-1 dhidi ya RB Salzburg katika UEFA

Kocha Graham Potter aanza maisha Chelsea kwa sare ya 1-1 dhidi ya RB Salzburg katika UEFA

Na MASHIRIKA

KOCHA Graham Potter, 47, alianza maisha kambini mwa Chelsea kwa sare ya 1-1 dhidi ya RB Salzburg ya Austria katika gozi la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) lililochezewa ugani Stamford Bridge mnamo Jumatano usiku.

Mkufunzi huyo wa zamani wa Brighton alitegemea pakubwa Raheem Sterling katika safu ya mbele na nyota huyo raia wa Uingereza akafunga bao katika dakika ya 48 baada ya kushirikiana vilivyo na Pierre-Emerick Aubameyang.

Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Chelsea kutandaza chini ya Potter aliyemrithi Thomas Tuchel ambaye alipigwa kalamu baada ya kikosi chake kufungua kampeni za UEFA msimu huu kwa kichapo cha 1-0 kutoka kwa Dinamo Zagreb kwenye Kundi E mnamo Septemba 6, 2022.

Chelsea kwa sasa wanavuta mkia wa Kundi E kwa alama moja baada ya AC Milan kutandika Zagreb 3-1 katika pambano jingine la Jumatano. Milan ambao ni wafalme wa soka ya Italia, watavaana na Chelsea katika mechi ijayo ya UEFA mnamo Oktoba 5, 2022 ugani Stamford Bridge.

MATOKEO YA UEFA (Jumatano):

AC Milan 3-1 Dinamo Zagreb

Shakhtar Donetsk 1-1 Celtic

Rangers 0-3 Napoli

Chelsea 1-1 RB Salzburg

Real Madrid 2-0 RB Leipzig

FC Copenhagen 0-0 Sevilla

Man-City 2-1 Borussia Dortmund

Juventus 1-2 Benfica

Maccabi Haifa 1-3 PSG

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Karua, Kalonzo wahudhuria sherehe ya Nassir kuapishwa

Aliyefukuza babake ashtakiwa

T L