• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 5:50 AM
Kocha Oyoo anoa nyota wa kesho

Kocha Oyoo anoa nyota wa kesho

NA ABDULRAHMAN SHERIFF

ALIYUKUWA kocha wa Thika Queens FC Joseph Oyoo ameamua kuanzisha timu ya wasichana wa umri wa miaka 10 hadi 15 kwa nia ya kuwakuza na kutwafanya wawe na vipaji vya kuchezea timu ya taifa ya Harambee Starlets.

Oyoo amesema jana Ijumaa kwamba ameonelea umuhimu wa kuanzisha timu ya wasichana wadogo apate kuwatengeneza na kuwa mastaa wakubwa kama walivyokuwa wanasoka wake wa awali ambao wengine hivi sasa wanacheza soka katika ngazi ya majuu.

“Nimeonelea nirudi kwa timu yangu ya Mombasa Olympic Ladies FC lakini nitaanzisha timu ya wasichana wadogo niwakuze sawa nilivyofanya kwa kina Mwanahalima Adam, Involata Mukosh, Nuru Mustafa, Winnie Achieng na wengineo amabao sasa wanacheza soka nchi kadhaa za nje,” akasema.

Oyoo amesema timu ya wachezaji wakubwa ya Mombasa Olympic Ladies FC inayoshiriki Ligi ya Taifa Daraja la Kwanza itabakia kusimamiwa na kocha Christine Nanjala na kamwe hatataka kumuingilia kwani anaamini anaweza kuifanikisha.

“Timu ya wakubwa ya Mombasa Olympic itaendelea kupata mafunzo kutoka kwa Nanjala kwani nina imani naye nilivyoondoka kwenda Thika ndiye atakayeiletea ufanisi. Nitasimamia timu wa wadogo nipate kuwainua chipukizi,” akasema.

Oyoo ni mmoja wa makocha waanzilishi wa soka ya wanawake nchini ambapo ametoa wachezaji wengi waliokuwa wakichezawakiwa kwenye timu ya Harambee Starlets lakini hajapata bahati ya kutambuliwa na maafisa wanaosimamia mchezo huo nchini na hatimaye pengine kumpa nafasi kuiandaa timu ya taifa.

  • Tags

You can share this post!

Nzoia Sugar juu, mashabiki wa Gor wakikemea kocha

Kiwanda kipya cha macadamia kuleta mabadiliko

T L