• Nairobi
  • Last Updated May 16th, 2024 8:50 PM
Kocha wa AFC Leopards ataka sheria za FIFA zifuatwe ligini

Kocha wa AFC Leopards ataka sheria za FIFA zifuatwe ligini

NA JOHN ASHIHUNDU

KOCHA wa AFC Leopards Patrick Aussems ameitaka kamati ya muda inayosimamia soka nchini ihakikishe sheria za FIFA zinafuatwa katika utendaji kazi wake.

Raia huyo wa Ubelgiji alisema hayo baada ya timu yake majuzi kurejea Nairobi bila kucheza dhidi ya Ulinzi Stars, hata baada ya kusafiri hadi Kericho kwa mechi hiyo Iliyopangwa kuchezwa Jumatano.

Leopards walikataa kuingia uwanjani baada ya wenyeji kukosa chombo cha kusaidia mtu ambaye amezimia (defibrillator).

“Ni jambo la kusikitisha kusafri saa sita barabarani kutoka Nairobi hadi Kericho, kugharimia wachezaji 30 bila kucheza kwa sababu wenyeji Ulinzi, kwa mara ya pili wamekosa vifaa muhimu kwenye ambulensi yao, nimeudhika sana,” Aussems aliandika kwenye mtandao wake wa Twitter.

Ulinzi walifanya makosa kama hayo mnamo Januari 8, ambapo Sofapaka walikataa kucheza baada ya kugundua vifaa kadhaa muhimu vilikosekana katika ambulensi iliyofika uwanjani siku hiyo.

Mechi hiyo ilitarajiwa kuanza saa tisa, licha ya Sofapaka walingojea kwa saa nzima, na huenda Leopards wakapewa ushindi kama Sofapaka.

Jinsi mambo yalivyo kwa sasa, Leopards wanashikilia nafasi ya 10 jedwalini kwa pointi 26 kutokana na mechi 20. Huku wakitegemea wachezaji wengi wasio na ujuzi, Leopards imeshinda mechi sita, kutoka sare mara nane na kushindwa mara sita, na mabao 21.

Ulinzi Stars wanashikilia nafasi ya 12 kwa pointi 25 lakini wamecheza mechi 19,ushindi mara sita, sare mara saba, kushindwa mara sita na mabao 15.

Kakamega Homeboyz, watetezi Tusker FC na Nairobi City Stars zinafuatana katika nafasi tatu za juu.

You can share this post!

Uingereza yavuruga mpango wa Abramovich kuuza Chelsea

WANDERI KAMAU: Ukatili wa bodaboda ulichora picha halisi ya...

T L