• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 5:50 AM
Uingereza yavuruga mpango wa Abramovich kuuza Chelsea

Uingereza yavuruga mpango wa Abramovich kuuza Chelsea

Na MASHIRIKA

MPANGO wa Roman Abramovic kuuza kikosi chake cha Chelsea umesitishwa baada ya bwanyenye huyo kuwekewa vikwazo na serikali ya Uingereza kutokana na ushambulizi unaofanywa na Urusi nchini Ukraine.

Abramovic ambaye amekuwa mmiliki wa Chelsea tangu 2003, aliweka wazi mpango wa kutia klabu hiyo mnadani baada ya tetesi za Bunge la Uingereza kumwekea vikwazo kufichuka.

Sasa ina maana kwamba Chelsea ambao ni mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) hawana kibali cha kuuza tiketi za mahudhurio ya mechi wala kunadi bidhaa au jezi za wanasoka wao.

Hatua hiyo inamnyima Abramovic ambaye ni raia wa Urusi fursa yoyote ya kupata fedha kutokana na kikosi cha Chelsea kinachoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Serikali ya Uingereza imesema itawapa Chelsea leseni spesheli itakayotoa mwongozo kuhusu jinsi mechi zilizosalia msimu huu zitakavyosakatwa, wafanyakazi na wachezaji watakavyolipwa mishahara na huku mashabiki walio na tiketi za kuhudhuria mechi zilizosalia wakipewa kibali cha kufanya hivyo.

Maduka ya kuuza bidhaa na jezi za wanasoka wa Chelsea tayari yamefungwa.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Chelsea warefusha mkia wa Norwich City ligini

Kocha wa AFC Leopards ataka sheria za FIFA zifuatwe ligini

T L