• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Kocha wa Ingwe awataka mashabiki wawe na subira

Kocha wa Ingwe awataka mashabiki wawe na subira

NA JOHN ASHIHUNDU

KOCHA Patrick Aussems amewataka mashabiki wa klabu hiyo wavumilie matokeo ya sare yanayofuata wakati huu ligi kuu ya Kenya imewaka moto.

Mbelgiji huyo alisema hayo baada ya timu hiyo kutoka sare 1-1 na Sofapaka kwenye mechi iliyochezewa Nyayo Stadium, Jumapili.

Leopards imecheza mechi 15 na kushindwa moja pekee, lakini kocha huyo amesema wachezaji wake wamejaribu wawezavyo ikikumbukwa kwamba timu hiyo inajumuisha wachezaji wengi wasio na ujuzi wa kutosha.

Akizungmza baada ya mechi hiyom, Aussems alisema timu yake itamaliza ligi katika nafasi nzuri, licha ya matumaini ya kutwaa ubingwa kufifia.

“Hii ni sare ya nane mfululizo, lakini kumbukeni hatujashindwa katika mechi mechi 15,” Aussems aliongeza.

“Hatuandikishi ushindi lakini tunaendelea kuandikisha matokeo ya kujivunia yatakayotuwezesha kumaliza ligi katika nafasi nzuri. Kuna change moto nyingi zinazowakumba wachezaji, na kwa hakika wanastahili heko kwa kujitahidi vilivyo.”

Katika mechi ya Jumapili, Leopards ilitoka nyuma na kuagana 1-1 na Sofapaka ambao ni mabingwa wa 2009, huku Nzoia chini ya Salim Babu ikiichapa Posta Rangers 1-0 ugani Kasarani Annex.

You can share this post!

MPC yaandaa matembezi ya kuhamasisha wanawake wajue haki zao

Baadhi ya wakazi wa Thika wafanya maandamano wakitaka Ruto...

T L