• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 12:11 PM
Kocha wa Ingwe kuteremsha uwanjani kikosi kikali dhidi ya K’Ogalo

Kocha wa Ingwe kuteremsha uwanjani kikosi kikali dhidi ya K’Ogalo

NA JOHN ASHIHUNDU

KOCHA Patrick Aussems ameahidi kuteremsha uwanjani kikosi imara cha kuvuruga matumaini ya Gor Mahia kesho Jumapili wakati wa pambano ligi kuu kati ya mahasimu hao wa jadi.

Raia huyo wa Ubelgiji kadhalika alifichua kwamba washambuliaji wake wawili – Victor Omune na Fasnami Ojo Olaniyi waliokuwa wakisumbuliwa na majeraha madogo sasa wako tayari kucheza mechi hiyo baada ya kupata nafuu.

Furaha ya kocha huyo ilipanda zaidi kufuatia kurejea kwa beki matata Tedian Esilaba ambaye amekuwa nje kwa wiki kadhaa kutokana na jeraha, lakini kulingana na repoti ya daktari Patrick Ngusale, wanasoka Kaycie Odhiambo Dan Sunguti na Jaffari Odeny wataendelea kukaa nje kutokana na majerah wanayouguza.

Omune na Olaniyi walijeruhiwa wakati wa mechi yao dhidi ya Kenya Commercial Bank (KCB) Jumapili iliyopita, lakini wamepata nafuu na tayari kabisa kurejea kikosini.

“Kila mtu anatamani kucheza Jumapili. Natarajia upinzani mkali kutoka kwa wapinzani wetu, lakini vijana wako tayari kuonyesha uwezo wao. Tuko tayari kabisa kwa lolote,” aliongeza.

Aussems anaamini ana kikosi imara cha kuibwaga Gor Mahia kwenye pambano hilo la debi ya 94 tangu zikutane kwa mara ya kwanza mnamo 1968.

Chini ya Aussems, Gor Mahia imeichapa Leopards katika fainali ya FKF Cup kupitia kwa mikwaju ya penalti mwezi Julai mwaka uliopita, kabla ya kufuatisha kichapo kingine cha 1-0 katika mechi ya ligi mkondo wa kwanza, pia mwaka huo huo.

Aussems ametoa mwito kwa mashabiki wa Ingwe wajitokeze kwa wingi kushangilia vijana wake ili wapate nguvu za kuandikisha matokeo mema.

Kocha huyo anatarajia kufanya mabadiliko machache kwenye kikosi chake kilichochapa KCB 2-1 Jumapili iliyopita, lakini mshambuliaji John Mark Makwata anayejivunia mabao matano katika mechi sita anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji.

Leopards haijawahi kushinda Gor Mahia tangu Machi 2016, lakini ushindi katika mechi ya leo utaiwezesha kupanda ngazi kutoka nafasi ya nane hadi ya 10 jedwalini, huku ikibakisha mechi sita kukamilisha msimu.

You can share this post!

Wito wazazi wakome kutumia kauli ya Magoha kuhepa kulipa...

Matiang’i aonya wanasiasa wenye ndimi za moto

T L