• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Wito wazazi wakome kutumia kauli ya Magoha kuhepa kulipa karo

Wito wazazi wakome kutumia kauli ya Magoha kuhepa kulipa karo

NA KNA

MWENYEKITI wa Chama cha Wakuu wa Shule za Sekondari nchini, (KESSHA), Kahi Indimuli, ametoa wito kwa wazazi ambao watoto wao wanajiunga na Kidato cha Kwanza walipe karo na wakome kutumia kauli ya Waziri wa Elimu, George Magoha kuwa walimu hawafai kuwatuma wanafunzi nyumbani kwa sababu ya karo kujitetea na kuhepa kuwajibika.

Bw Indimuli ambaye ni Mkuu wa Shule ya Wavulana ya Machakos, alisema kuwa wazazi wengine sasa wanakataa kulipa karo wakidai kuwa Waziri Mogoha alisema kila mwanafuzi ajiunge na Kidato cha Kwanza.

Hata hivyo, aliwataka wazazi wanaokosa kulipa karo wawe na sababu ya kutofanya hivyo.

“Katika kutekeleza sera za serikali, lazima pia tupate msimamo ifaayo kwa nini mzazi hawezi kutimiza wajibu fulani. Tunataka wazazi waeleze ni kwa nini hawawezi kulipa karo na wala si kutumia kauli ya waziri kama kisingizio. Hilo halikubaliki,” akasema Bw Indimuli.

Kadhalika, alibainisha changamoto nyingine inayowakabili ni wazazi ambao wanajaribu kuwabadilisha watoto wao kutoka shule moja kwenda nyingine na baadaye kubadili mawazo na kutaka kurejea shule ya awali.

“Baadhi ya wazazi wanabadili msimamo wao na kutaka kuwarejesha wanao katika shule za awali baada ya kugundua kuwa ilikuwa bora,” akasema Bw Indimuli.

You can share this post!

Ruto ameingia baridi – Mucheru

Kocha wa Ingwe kuteremsha uwanjani kikosi kikali dhidi ya...

T L